Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 26, 2019

Waziri Hamad Rashid atoa neno kwa wagonjwa!

Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed amewataka wagonjwa wanaofika hospitali mbali mbali Nchini kutoa taaarifa pindi  wanapofikwa na jambo la udhalilishaji wa aina yoyote.

Aliyasema hayo leo  huko Ofisini kwake Wizara ya afya Mnazi Mmoja, wakati  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taarifa ya daktari wa Hospitali ya Chake kutaka rushwa ya ngono kwa mgonjwa.

Amesema kitendo hicho sio kizuri kwa taifa kwani kinawafanya wagonjwa kuwa  na wasiwasi ambao wanapohitaji matibabu wakati wanapofika hospitali.
Aidha amesema Serikali haikufurahishwa na kitendo  hicho hivyo kwa kushirikina na Wizara ya Afya wamechukua hatua  ya kumtaka muhusika kutoa taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Pia Mhe. Hamad amesema katika kupambana na tatizo hilo Serikali imeamua kumsimamisha kazi daktari huyo ili kupitisha uchunguzi na kuchukua hatua za sheria ikiwa atathibitishwa kufanya udhalilishaji huo.

Hata hivyo Waziri huyo amewataka akina baba kushirikiana na wake zao wakati wanapokwenda Hospitali kimatibabu ili kuepuka vitendo vya udhalilishaji.

Akizungumzia suala la mshahara kuhusu daktari huyo Mkurugenzi Mtendaji Utumishi Wizara ya afya Ramadhan Khamis Juma amesema kwa sasa analipwa nusu mshahara hadi kukamilika uchunguzi na ikigundulika kufanya hivyo atasimamishiwa mshahara wake.

No comments :

Post a Comment