Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Thursday, January 30, 2020
MAALIM SEIF ACHUKUWA FOMU YA KUGOMBEA UENYEKITI TAIFA WA ACT WAZALENDO!
MSHAURI Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amechukuwa fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa.
Maalim ambae alikuwa Katibu Mkuu wa CUF kabla ya kuingia ACT Wazalendo alichukuwa fomu hiyo jana katika ofisi za chama hicho Vuga na kukabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu wake Dorothy Temu.
Akizungumza mara baada ya kuchukuwa fomu hiyo Maalim Seif alisema kuwa ameomba nafasi hiyo ili aweze kutoa mchango wake katika kukiimarisha na kukuendeleza chama hicho.
Alisema kuwa anaamini kabisa ana uwezo wa kutosha wa kuongoza, hivyo iwapo wanachama watamchaguwa ataweza kuendeleza uomja, mshikamano na mafahamiano miongoni mwa wanachama na viongozi wenyewe.
“Mimi ni mwanachama hai, nimeamuwa kutumia haki yangu ya kikatiba kuomba nafasi hii ya uongozi kitaifa, kama sitotumia haki hii baadhi ya wanachama hawatonifahamu na najuwa kama bado wanaimani na mimi na hivyo sikutaka kuwavunja moyo”, alisema.
Hata hivyo alisema kuwa nafasi ambayo ameiomba haihusiani na utendaji, Mwenyekiti wa chama ni nafasi ya uongozi, ambayo anahakika kama atapata ridhaa ya wanachama wake ataweza kuendeleza utamaduni na
nidhamu na kufanyakazi kwa mashirikiano.
“Naamini kabisa kwamba uongozi wangu na wenzangu tutajenga chama chenye umoja na mashirikiano”, alisema Maalim Seif.
Kuhusu kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 alisema kuwa ni mapema kuzungumzia hilo na kikubwa ambacho kwa sasa atakizungumza ni kuhusu kuchukuwa fomu za uongozi wa ndani kama ambavyo chama
kilivyotangaza.
Alisema kuwa kusema kama atachukuwa au kutokuchukuwa hilo ataweza kulisemea wakati muda muafaka utakapofika lakini kwa sasa lililopo mbele yao ni nafasi za uongozi wa ndani.
“Leo nimekuja kuchukuwa fomu ya uwenyekiti wa taifa wa chama, wakati wa kuchukuwa fomu za urais bado chama hakijatangaza na nitaweza kutoa maamuzi wakati ukifika”, alisema Maalim Seif ambae ameshagombea kwa
vipindi vitano pasipo na mafanikio.
Mapema Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho Dorothy Temu aliwataka akinamama na vijana kujitokeza kuchukuwa fomu kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ili waweze kushiriki katika kujenga chama chao.
Zoezi la uchukuaji fomu kuomba nafasi za ndani za uongozi lilianza Januari 27 mwaka huu, litamalizika Febuari 27 mwaka huu, ambapo mpaka sasa Maalim Seif ndie mgombea pekee aliechukuwa kuwania nafasi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

No comments :
Post a Comment