
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020/25 mgombea Ubunge Jimbo la Kawe Askofu Gwajima kwenye mkutano wa Kampeni wa Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika katika Viwanja vya Muwembe Yanga Jijini Dar es salaam leo Septemba 05,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi katika Viwanja vya Muwwembe Yanga Jijini Dar es salaam leo Septemba 05,2020.
No comments :
Post a Comment