NAENDA KUOA PEMBA!
MAJIBU: WAPI POSA UPELEKE....!!!
Kwanza nakuja na hoja, shairi langu la jana,
Kukuita wa viroja, kweli nilikosa sana,
Sisi sote Wa-Unguja, siache kutaniana,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Hebu kidogo subiri, Pemba tutafuatana,
Kule kwa vichinchiri, kunasifikana sana,
Utadhani wa hariri, wametameta mchana,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Nilikuenda na Jabiri, hakuondoka kijana,
Nikaita askari, pamoja na kamishina,
Alimaliza dinari, akawa hana dhamana,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Wapi posa upeleke, wapi wewe watamani,
Nia usiwe mpweke, hata huyo wa Kojani,
Kama waweza mateke, basi bora kaposeni,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Muulize babu Haji, alioa Shengejuu,
Na sote tukamuhoji, ilikuwaje mkuu???
Kafilisika mtaji, kimwana yake makuu,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Hata kile cha usiku, wakila kule Bwejuu,
Bibi hupika kwa siku, kama waziri mkuu,
Kama sio yule Chiku, wangekula wajukuu???
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Usijali Wa-Unguja, au ni wa kule Pemba,
Kama anakidhi haja, hata akiwa mshamba,
Bora awe wa faraja, ila asiwe mwembamba,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Nilikueleza jana, nenda hata kule China,
Hutopata orijina, si sawa na kuwa huna,
Japo hawapaki hina, wanamacho ya aina,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Sitaki andika tena, najiogopea sana,
Kwa lile shairi jana, naambiwa natukana,
Ukeshampata mwana, unisamehe kijana,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Kukuita wa viroja, kweli nilikosa sana,
Sisi sote Wa-Unguja, siache kutaniana,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Hebu kidogo subiri, Pemba tutafuatana,
Kule kwa vichinchiri, kunasifikana sana,
Utadhani wa hariri, wametameta mchana,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Nilikuenda na Jabiri, hakuondoka kijana,
Nikaita askari, pamoja na kamishina,
Alimaliza dinari, akawa hana dhamana,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Wapi posa upeleke, wapi wewe watamani,
Nia usiwe mpweke, hata huyo wa Kojani,
Kama waweza mateke, basi bora kaposeni,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Muulize babu Haji, alioa Shengejuu,
Na sote tukamuhoji, ilikuwaje mkuu???
Kafilisika mtaji, kimwana yake makuu,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Hata kile cha usiku, wakila kule Bwejuu,
Bibi hupika kwa siku, kama waziri mkuu,
Kama sio yule Chiku, wangekula wajukuu???
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Usijali Wa-Unguja, au ni wa kule Pemba,
Kama anakidhi haja, hata akiwa mshamba,
Bora awe wa faraja, ila asiwe mwembamba,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Nilikueleza jana, nenda hata kule China,
Hutopata orijina, si sawa na kuwa huna,
Japo hawapaki hina, wanamacho ya aina,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
Sitaki andika tena, najiogopea sana,
Kwa lile shairi jana, naambiwa natukana,
Ukeshampata mwana, unisamehe kijana,
Wapi posa upeleke, kwake unomtamani.
/Kutoka Zanzibar!
NAENDA KUOA PEMBA!
Naenda kuoa Pemba, msichana wa Kojani
Yule anaejipamba, kwa mitandio kichwani
Aongea kwa kutamba, na lafudhi ya kipwani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Kojani nikimkosa, natafuta Mkoani
Niweze peleka posa, ili nipate mwandani
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nikaoe Wete, nikikosa Mkoani
Nende nimvishe pete, yule ninomtamani
Tena niwazidi kete, hao wangu washindani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nende Shengejuu, tena kule ndani ndani
Nipate mwenye nafuu, aniliwaze moyoni
Kwa maji ya karafuu, anikande maungoni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Naulizia Kengeja, naomba nipelekeni
Kwa wanouza vileja, tosi halua ubani
Namuhitaji mmoja, sisikii na sioni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Wakazi wa Chakechake, hasa wa hapo mjini
Msije nipiga teke, nikafia baharini
Msiniache mpweke, niozesheni jamani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Ndugu zangu wa Kianga, naomba nipokeeni
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni
Kama nyumba nitajenga, hata pale Mnarani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nisogee Wingwi, sababu wanithamini
Najua pale sipingwi, hata kama masikini
Sitozamishiwa Nungwi, nikiwa na hali duni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Sebu pasahau Konde, napapenda kama nini
Taenda hata kwa mbinde, kwa uwezo wa Manani
Nahitaji anikande, nitaporudi kazini
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Hapa kituo niweke, kalamu niweke chini
Wapi posa nipeleke, mawazo tele kichwani
Nioe nifurahike, raha ya ndoa ndoani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Aongea kwa kutamba, na lafudhi ya kipwani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Kojani nikimkosa, natafuta Mkoani
Niweze peleka posa, ili nipate mwandani
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nikaoe Wete, nikikosa Mkoani
Nende nimvishe pete, yule ninomtamani
Tena niwazidi kete, hao wangu washindani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nende Shengejuu, tena kule ndani ndani
Nipate mwenye nafuu, aniliwaze moyoni
Kwa maji ya karafuu, anikande maungoni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Naulizia Kengeja, naomba nipelekeni
Kwa wanouza vileja, tosi halua ubani
Namuhitaji mmoja, sisikii na sioni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Wakazi wa Chakechake, hasa wa hapo mjini
Msije nipiga teke, nikafia baharini
Msiniache mpweke, niozesheni jamani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Ndugu zangu wa Kianga, naomba nipokeeni
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni
Kama nyumba nitajenga, hata pale Mnarani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nisogee Wingwi, sababu wanithamini
Najua pale sipingwi, hata kama masikini
Sitozamishiwa Nungwi, nikiwa na hali duni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Sebu pasahau Konde, napapenda kama nini
Taenda hata kwa mbinde, kwa uwezo wa Manani
Nahitaji anikande, nitaporudi kazini
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Hapa kituo niweke, kalamu niweke chini
Wapi posa nipeleke, mawazo tele kichwani
Nioe nifurahike, raha ya ndoa ndoani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
/Mtunzi kutoka Muscat , Oman.
Kwa tunzi za kabla click here below:
TUNAKARIBISHA MASHAIRI, UTENZI, FEATURE ARTICLES, PHOTO EVENTS, NEWS, N.K KUTOKA KWA WASOMAJI WETU, LAKINI TUNAO UHURU WAKUBADILISHA INAPPROPRIATE WORDS ZILIZOTUMIKA BILA YA KUTAKA RIDHAA YA MTUNGAJI. KUWASILIANA NA SISI, TUMIA EMAIL: znzkwetu@gmail.com
ReplyDelete-ZNK Admin
Good job ZNK!
ReplyDelete