Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 16, 2012

BI SALMA SAID AFAFANUA JUU YA JUMA KIBWANA!
Asema:
Nia ni kumsaidia mwenzetu
Saidia kwa njia yoyote uiwezayo 

Zanzibar, Tanzania
August 16, 2012.
Bi Salma Said ambae ametoa tangazo kwa wote wenye nia na uwezo wa kusaidia, kumsaidia Bw. Juma Kibwana wa Kikwajuni ambae ni mwenye kukabiliwa na matatizo na shida tele za kiafya hivi sasa, amefafanua leo kwenye mtandao wa Mzalendo.net  na kuandika kama ifuatavyo:

"salma 16/08/2012 kwa 9:42 mu • Jibu
Waalaykum Salaam.
Nadhani sitaweza kumjibu mtu mmoja mmoja lakini nitajibu yale maswali ambayo hanahitaji ufafanuzi na nitajibu kwa kadiri nitakavyoweza ingawa mengine sitakuwa na uwezo nayo bali nitajibu yale tu ambayo nina uwezo nayo inshallah.


Sheikh Zahor unasema huyu jamaa sio mzee ni kijana wa age zenu ni kweli ni kijana hana uwezee huo hafiki hata miaka 50 lakini yeye ni tofauti na wewe au mie kutokana na kuwa yeye sasa ni mgonjwa yupo kitandani na hivyo basi tofauti ipo hapo kwamba kwanza ni mgonjwa na pili ni kuwa hana uwezo.
Sheikh Zahor pia umetaka kujua juu ya msaada unaohitajika kwa huyu ndugu yetu Juma Kibwana na sio kitwana kama nilivyoandika mwanzo naomba radhi kwa hilo. kwa hakika anahitaji msaada wowote utakaokuwa nao wewe mtoaji lakini tayari tumeshapata wheel chair kutoka kwa ndugu zetu wanaoishi Uingereza tumepata kigari kimoja na hivyo kwa tatizo hilo Alhamdulillah lakini sasa kwa wale wenye uwezo wa kutoa fedha basi kwanza tumsaidie fedha kwa ajili ya kutakiwa matibabu lakini pia kutokana na hali yake kama mnavyomuona bila ya shaka hata fedha ya matumizi inahitajika kwa kuwa yupo ndani na hawezi kutoa nje akafanya kazi anategemea ndugu zake ambao nao bila ya shaka wanahitaji kusaidiwa.



Amma hayo uliosema kuwa hana mke wala hana mtoto haioneshi ukubwa wa tatizo la kuhitaji kusaidiwa kama unavyosema. hilo ikiwa ni maoni yako au mtazamo wako unakhisi sio hoja wala halina uzito hilo sawa siwezi kukupinga wala siwezi kukataa mawazo yako naweza nisiyakubali lakini nitayaheshimu inshallah.
Lakini jambo la msingi ni kuwa mtu mgonjwa mwenye uwezo na akawa na mke na watoto wa kumtazama na kumsaidia na mtu mwengine mgonjwa ambaye hana mke hana watoto na watu alionao hawana uwezo bila ya shaka yoyote itakuwa ni tofauti wawili hawa na hicho ndio nilichokusudia kukieleza. lakini nadhani kwa wakati huu hatuna haja ya kuendeleza malumbano na tunachohitaji ni msaada wa huyu ni mgonjwa inshallah hayo mambo mengine nadhani tuyawache kwa sasa .
Amma unapotaka kujua zaidi kuhusiana na suala hili ni kuwa kama nilivyoeleza awali kwamba huyu ni kijana ambaye anahitaji msaada. na kuhusu mpiganaji nadhani ndugu yangu Zahor hujasoma vyema nimeandika kwamba ni mpiga picha maarufu alikuwa akifuatana na Eddy Taimuri Saleh Juma ambaye ndiye aliyekuwa rafiki yake sana, kwangu mimi zaidi ni kutaka asaidiwe mambo yake nadhani aachiwe mwenyewe na kwetu sisi kwa anayeguswa na ugonjwa wake amsaidie bila ya kutazama huko nyuma alifanya nini au yeye ni mtu wa aina gani, ninapochukua dhamana ya kuwaombea watu misaada huwa sitazami huyu ni nani na yule ni nani natizama zaidi tatizo la mtu na ugonjwa wake na pia jee familia yake inamudu au haimudu nikishapata ushahidi wa hayo basi mimi najibebesha dhamana la kumsaidia mtu huyo,
Na kama nilivyosema huko awali kwamba mimi huyu simjui in details kama ambavyo hao wengine sikuwa nawajua bali naletewa na jamaa zao au naletewa na Bi Abeid nitangaze na nikifuatilia au nikiridhika na ushahidi wa kuwa anahitaji msaada basi huwa nawaombea msaada.
Lengo ni kuwatangazia ndugu na jamaa muweze kusaidia na kutoa sadaka zenu kwa watu amabo kweli wanahitaji msaada hasa kwa wale ambao hawajiwezi na hawana uwezo wa kujitibu. Huu mchango sio wa harusi wala sio wa kufanya karamu bali ni mchango wa mgonjwa ambaye hana uwezo kwa hivyo ili nikupeni moyo na nikuaminisheni kwamba fedha zenu mnazotoa hazipotei ni kuwa nakuombeni ikiwa mtu anahitaji kusaidia basi aamini kwamba fedha mnazotoa zinafika kwa mlengwa kwa kuwa hili jukumu nalifanya kwa imani ya kutarajia ujira kutoka kwa ALLAH basi najitolea kufanya hiyo kazi na ili kwa wale ambao wana shaka na fedha zao napenda waamini kwamba shilingi ya mtu haiwezi kupotea kwa jambo jengine lolote kinyume na malengo yaliokusudiwa. Na ndio maana huwa nakwenda kukabidhi hizo fedha na kiasi cha fedha zilizotolewa lakini pia kwa kuonesha picha kama ushahidi zaidi ya hivyo wallahi sijui tena lakini inshallah kwa kuwa nia yangu ni kutaka ujira kwa ALLAH basi inshallah inshallah imani yangu ibaki hapo hapo yarabbi
SALMA SAID."

Pamoja na maelezo hayo ya Bi Salma, yule mwanakada wa ukumbi wa Mzalendo.net anaejulikanwa kwa jina la upiganaji (nom de guerre) kama Said Sudi alionekana akitokwa na machozi katika Ramadhani hii pale alipokuwa akiandika kwenye ukumbi huo kuwa "Jamani, tujitahidini tumsaidie mwenzetu, kwani nchi yetu ndio haina msaada. The rich are getting richer and the poor are getting poorer – day in day out. Na tuliobakia tumezama kwenye siasa zisizokuwa na maana!"
Ukitaka kusaidia, basi peleka mchango wako kwa watu hawa wafuatao:

Salma Said,
P. O. Box 1442,
Tel:                         +255 (024) 223 5219        
Mobile:                         +255 777 477 101        
E-mail: muftiiy@yahoo.com

Hassan Mussa Khamis
Mobile:                         +44 7588550153        
email: hassan.mussa@gmail.com
United Kingdom

Hassan Othman
Zanzibar-Canadian Diaspora Association
(ZACADIA)
Phone:             +1.416.438.7857    
Email: zacadiaw@gmail.com
Toronto, Canada.

Na Geo Kimbi /Wagagagigikoko News Network


No comments :

Post a Comment