HASSAN NASSOR MOYO APIGWA FULL STOP IKULU ZANZIBAR!
Hassan Nassor Moyo, mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar na miongoni mwa waasisi wa ASP na baadaye CCM [mwanachama NO.7 wa CCM] amekataliwa kumuona Rais Ali Mohammed Shein takriban mara mbili hadi tatu mfululizo kwa siku za hivi karibuni.
Sababu kubwa zilizotolewa na Ikulu na baadaye Rais mwenyewe ni kuwa ‘yuko busy na kazi muhimu za kiserikali’.
Moyo: Enzi zake, kila wakati akiwa pembezoni mwa Nyerere na Karume
Simply, it’s not fair union!
Sijui kama watendaji wa Ikulu wanajua kuwa Urais wa Shein umetokana na kauli ya Moyo na marehemu Abdullah Said Natepe — wao ndio waliokwenda kwa Kikwete, then kuwashawishi CCM — NEC na CC kuwa Shein ndio ‘chaguo lao; na ndio chaguo la CCM na chaguo la Wazanzibari’.
Katika hili mimi ninalijua vizuri sana. Siku moja wakati ule bado Natepe anaumwa (mwanzo Muhimbili) — mimi na wenzangu wawili watatu — tulikwenda kumuona Mzee Natepe; na Moyo alituuliza ‘mnafikiri Rais wa Zanzibar atakuwa nani, au nyinyi mnamtaka nani”.
Sote tulinyamza kimya! [wakati ule tayari kuna watu wameshatajwa na wameshaanza kupiga kampeni za Urais]. Mzee Moyo na Napete walitumbiwa kuwa ‘mgombea wetu sisi wazee bado hajulikani na hajatajwa”; tetesi zilikuwa zimewiva kuwa Dr.Shein huenda atachukua form za kugombea Urais wa Zanzibar – na hilo ndio ilikuwa chaguo la Mzee Hassan Nassor Moyo-Natepe.
Leo Mzee Moyo anafukuzwa Ikulu na watu wasiojuwa fadhila!
Bw. Hassan Nassor Moyo amekuwa na msimamo usiotetereka juu ya mabadiliko ya Muungano. Tujue kuwa hili ndio tegemeo letu Wazanzibari, tunamtegemea sana Mzee Moyo kama ndio sauti yetu nzito ya kupata haki yetu ndani ya Muungano; akidhalilishwa namna hii – TUMEKWISHA, na hii ndio kampeni inayoendelea sasa ndani ya SMZ na CCM-Zanzibar.
Hata hivyo, Mzee Moyo pamoja na juhudi zake nzuri z akutaka kuikomboa Zanzibar kwa uzoefu wa siasa za ASP, CCM, Muungano na siasa za Zanzibar — Mzee wetu huyu kipenzi amekosa strategy na planners wazuri kisiasa.
Kosa moja kubwa analofanya Mzee Moyo ameegemea sana na akina Salim Bimani na watu wa CUF – hii iko wazi, so yoote anayosema inaonekana ni ‘sauti ya CUF’. That’s wrong. Ilikuwa Mzee Moyo abaki na nguzo yake ile ile CCM; na sio kujinasibisha sana na CUF – CUF ni wavurugaji na si watu wazuri sana katika mapambano ya siasa za Zanzibar kama watu wanavyoaamini.
Kosa la pili analofanya Moyo – ameungana sana na hawa mrengo wa kushoto akina Makomredi wa Zanzibar – akina Ahmeid Rajab na wenzake amewaamini sana – hawa pia sio watu wazuri aghlabu si watuwazuri sana katika harakati za kuleta manufaa ya Zanzibar – ni watu wabinafsi, wenye khulka ya kibagzui guzi – unaweza kukosa kusikilizwa au kupata haki zako za msingi kama utajumuika na akina hawa MAKOMREDI AU CUF.
Wenyewe wanaweza kuwa wakali na kukaidi kama ilivyo ada yao, lakini wasikatae – Ramadhan yote makomredi wamefuturu na kumualika Mzee Moyo akiwemo mgeni wao Hashil Seif aliyezuru Zanzibar – Mzee Moyo yeye anajua kuwa system ‘can track and crack his communication’ au nyendo zake. Na ukweli hasa hili au mambo haya ndio yamemfanya Dr.Shein asikubali kuonana naye Mzee Moyo. Siye tena Moyo tunayemjua sisi enzi zile za ASPYL (youth).
Dr.Shein hana tatizo kabisa na Mzee Moyo ila watu waliomzunguka Moyo kwa sasa ndio kikwazo. Mfano mzuri ni kuwa press conference aliyoifanya pale hoteli ya Rumaisaa, karibu na Beit el Yamin walioandaa press conference ile ni CUF na wapambe wao akina mtoto wa marehemu Riamy; mtoto wa Said Gwiji na yule kijana anayeitwa Bajuber n.k
Waandishi walioitwa na kuhoji na kuuliza wote wamepangwa na kulishwa maswali ili waulize vile wanavyotakiwa na ipatikane jawabu sahihi – muungano wa mkataba (hakuna kitu kama hicho duniani ila CUF ndio wanaokijua).
Mzee Moyo anajimaliza na mfumo wa siasa Tanzania na Zanzibar utammaliza.
Labda kama atajirekebisha huenda ataonana na Rais Shein tena na tena hivi karibuni; lakini doa limeshaingia na halitoki kwa jik wala harita.
Inauma sana sana kuona kuwa Zanzibar tunahsindwa kuwa na agenda ya pamoja na strategy nzuri ya kuipata nchi yetu – ujuaji na kujinasib tu: ndio hawa akina Ahmeid Rajab wanababaisha watu na kuandika wasichokijua! Allah Karim.
Tunazidi kuikosa Zanzibar kwa kuwa na fikra za kijazba jazba: tumesema kuwa utoaji wa maoni — Muungano haumo wananchi ndio wanazidi kuambiwa wasema ‘muungano wa mkataba’.Tutakuja kujuta.
Chanzo: Mzalendo.net
No comments :
Post a Comment