MWENENDO WA SENSA UKWELI HAUJASEMWA
KAMA LENGO NI KURIDHISHANA HEWALA LAKINI…..
KAMA NI KUPATA TAKWIMU SAHIHI HILO NI ARDHI NA MBINGU FUATILIENI.
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Nchini Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Baloi Seif Ali Iddi akikiendesha Kikao cha Saba cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mjini
Dar es slaam.
(Vikao vingi aandika Nd. Zdaima ni ishara ya kuwa mambo hayaendi vizuri)
Huwezi ukaamini kama vile ni sinema tulizozoweya ( za KIHINDI ) siku zote “stering” ama ( hero ) hafi au hauwawi, ndivyo lilivyo hili la sensa mwaka huu.
HISTORIA FUPI KABLA YA SENSA.
Waislamu na taasisi zao bara na visiwani waliadhimia kususia sensa ( sio wote) kwa madai haya.
1. Kuzuka takwimu za mashirika ya dini na serikali kutowa takwimu feki na kuiomba serikali kukanusha au kuthibitisha lakini iliwadharau waislamu na hatimae waislamu wakasindikiza kipengele cha dini kiingizwe ili kuondoa utata serikali kama kawaida iliwadharau waislamu.
2. Kipengele cha dini ni miongoni mwa vipengele muhimu na kinakubalika kimataifa kama item ya kupanga mahitaji ya watu kwa nini Tanzania ( mfumo kristo ) wao walishasema ni wengi lengo ni kuhalalisha wingi wao katika kila ofisi ya serikali .Waislamu kama kundi la jamii hili wanalijua.
3. Serikali kupitia idara ya takwimu ilitakiwa itaje sensa ya mwisho ambayo iliingiza kipengele cha dini na matokeyo yake yakoje iligwaya.
Baada ya serikali kugoma kusikiliza ushauri wa taasisi za kiislamu ilitumia hila za kuwagawa waislamu Taasisi na Bakwata .na wakafanikiwa kuwatoa bakwata katika ile shura ya waislamu dhidi ya serikali.(mgawanyiko)
- Serikali kutumia vitisho
-Matamko na hilba za viongozi wa siasa
- kuwaweka watu ndani ( Singida, Tanga , Daresalaam n.k)
HALI HALISI WAKATI WA SENSA.
Ukweli ni kwamba licha ya serikali na vyombo vya habari kufanya propaganda waislamu wengi hawakuitikia wito na inafanywa isionekane hivyo.
Ingia mitaani ufanye “Interview) utagunduwa tofauti na yanasemwa na makarani na pia vyombo vya habari.
- watu wamebadilisha staili ya kugomea hasa mjini kutoka kufunga milango hadi kuwanyamazia kimya makarani na kutowa idadi feki na majibu ya mkato ( no clarity)
- Makarani na masheha wanazuga hawasemi wanayokutana nayo. hapa ni kwamba makarani hupita na kukuta nyumba iko wazi akianza kuuliza watu hutokomeya bila kurupushani hasa nyumba zenye vijana wa kiume . nimeyaona sehemu nyingi za Bububu, Magogoni na jimbo la mfenesini katika ufuatiliaji wangu. hapa hakuna kubishana baina ya pande mbili lakini hakuna kushirikiana.( no cooperation)
KWA NINI VIKAO NI VINGI NA MWITO WA KUSHIRIKI NI MWINGI?
wale wanaojuwa mambo wanajua kiukweli zoezi linakwama na inafanywa watu waamini kwamba mambo ni shwari jamani kwa faida ya nani? hapa sio ishu nyumba ngapi zimekubali lakini ni nyumba ngapi zimotowa takwimu sahihi na jee hili hao makarani wanaliripoti ? sensa imekosa sifa.
UHALISIA WA MAMBO
- Hakuna tawimu sahihi zinazotolewa
- Baadhi wamekataa kuhesabiwa kabisa soma (zanzibar leo TRH 29/8/2012) kaya 600 sikwambii hawa ambao hawajaripotiwa kwa sababu maalumu fuatilia Nugwi, Bumbwini, chwaka , uzi, maeneo mengi jimbo la magogoni, bububu n.k) maeneo ni mengo
-kutoripotiwa baadhi ya matukio muhimu kama mkakati
-serikali kuendelea kuwatisha watu na kutishia kuwafunga wakati zoezi linaendelea.
-Kuna mgawanyiko wa watu kuhusu kushiriki wengine wanaendelea na shughuli zao na wala hawahesabiwa.
_ vifaa baadhi ya maeneo vimechelewesha zoezi na watu kukata tamaa.
SIFA ZA KUFANIKISHA SENSA.
-Kuwe na maelewano na Ushirikiano Vipi yapo ?
- Kuwe na ukweli
- Kusitumike vitisho wala nguvu ( wahazabe wamepewa nyama ya punda jee waislamu wao vipi si watu ? hawakusikilizwa.
-Kusiwe na kususiana na kushutumiana ikiwepo hali hii hakutokuwa na ” clarity ” katika takwimu jamani yote haya yapooooo.
- N. K.
SERIKALI HAIJUWI IDADI YA WATU, KAYA au WAKAZI NINI KINAFANYIKA .
Sensa ni zaidi ya hayo ndio maana serikali inahangaika .
- Kama ni kaya tu basi sheha anazo zote na hata watu wanaoishi ingawa wengine huzaliwa , kuhama na kuhamia.
-Kama ni watu tu wangejulikana japo kama si kwa sensa wakitaka watawajuwa bila watu wenyewe kujijuwa -mbona vitambulisho wanajuwa nani apewe nani asipewe wala haifanywi sensa.
- Kama ni wakaazi ile idadi ya vyandaruwa haitoshi au ule mradi ushakwisha ?
MWISHO.
Miminaona vyovyote itakavyokuwa tayari sensa ilikuwa na dosari kabla ya kuanza, wakati inaedelea na baada ya kwisha.Kabla ya kuanza kulikuwa na malalamiko na maazimio ambayo mpaka sasa hayajesha.
Wakati inaedelea kuna matatizo mengi ya dhahiri na yanayofichwa hakuna usahihi katika zoezi.
Baada ya kwisha itakuwa ndio zaidi hapa Tanzania siku zote la kweli halisemwi serikali imekuwa “stering” wa kihindi hauwawi . licha ya dosari zilizojitokeza ,zinazoendelea na zijazo kamwe hazitobadilisha msimamo madhali ndivyo alivyo stering wa kihindi lakini serikali na sensa sahihi ni vitu viwili tofauti. tusijidanganye wenyewe. ikiwa wahazabe serikali imotowa millioni 5 kwa ajili ya nyama ya punda ili waache mgomo na kushiriki sensa itakuwaje jamii ya waislamu iwe hata robo moja tu ya watu wote wasiathiri sensa halafu tanalazimishwa tuamini sensa inakwenda vizuri ? hili litaisaidia vipi serikali ?
Hili la sensa mwaka huu tuiite move ” THE SENSOR THE HERO THE GOVERNMENT THE SUPER HERO ”
Nawasilisha.
Chanzo: Mzalendo.net
No comments :
Post a Comment