dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 7, 2012

MSIMU WA KARAFUU KUANZA‏ ZANZIBAR

Na Juma Mohammed, MAELEZO Zanzibar

Wizara ya Biashara ,Viwanda na Masoko imetangaza kuanza kwa msimu mpya wa ununuzi wa karafuu kutoka kwa wakulima kwa kuendelea kununua kwa wakulima kwa bei ya shilingi 10,000/= kwa kilo katika msimu wa mwaka 2012-2013.

                                           Mkulima wa Zao la karafuu katika Kijiji cha Pandani akianika karafuu zake 

Katika Taarifa yake, Waziri wa Wizara hiyo, Nassor Ahmed Mazrui alisema kiwango hicho cha bei kitapanda iwapo bei ya kuuzia nje itaongezeka.

“Kwa upande wa bei ya kununulia karafuu kutoka kwa wakulima, Serikali imezingatia kwa undani hali ya mwendo wa bei ya zao hilo katika masoko ya nje na kuona kuwa hakuna matarajio mazuri ya kuinuka kwa viwango vya bei vilivyopo hivi sasa” Alisema Waziri huyo.

Waziri Mazrui alisema sababu inayochangia hali hiyo ni kuwepo kwa matarajio ya vuno kubwa katika nchi ya Indonesia ambayo ni mzalishaji mkubwa wa karafuu duniani.

“Hata hivyo, Licha ya matarajio ya hali ya soko kutokuwa nzuri kwa msimu ujao,Serikali bado itaendelea kuongozwa na misingi ya kulipa asilimia 80 ya bei ya kuuzia nje kwa msimu ujao” Alisema Waziri Mazrui.

Mwaka jana Serikali iliongeza bei ya ununuzi wa karafuu kwa wakulima kutoka shilingi 3,500/= kwa kilo hadi kufikia shilingi 10,000/= kwa kilo ambapo pamoja na uamuzi huo, Serikali ilitangaza mambo mawili ambayo ni kumlipa mkulima asilimia 80 ya bei ya kuuzia nje na kuiongeza kila bei ya kuuzia nje itakapoongezeka.

Waziri huyo alitaja jambo la pili kuwa Serikali haitoshusha kiwango cha bei kilichotangazwa hata pale bei ya kuuzia nje itakaposhuka kwa msimu unaohusika.

Alisema msimu wa mwaka jana, Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar(ZSTC) lilifanikiwa kununua karafuu zote kutoka kwa wakulima hatua iliyowezesha kununua tani 4,822 zenye thamani ya shilingi 72,100.0 milioni kiwango ambacho ni rekodi ya kihistoria kwa zao la karafuu Zanzibar.


Waziri Mazrui alisema msimu wa ununuzi karafuu ulifungwa Julai 20 mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ambapo ZSTC ilitakiwa kutimiza wajibu wa kisheria wa kufunha hesabu zake kwa msimu wa 2011-2012 na kufanya tathimini ya mali zake.

Waziri huyo alisema pia ZSTC ilitakiwa kufanya tathimini ya soko la nje la kuuzia karafuu kwa madhumini ya kubainisha kiwango cha bei ya kununulia karafuu kutoka kwa wakulima.

Waziri Mazrui ameongeza kwa kuwataka wananchi na hasa wakulima wa zao la karafuu kuipa ushirikiano Serikali kama ilivyokuwa katika msimu uliopita kwa kuitikia katika sjuala la uvunaji na uuzaji karafuu ZSTC.

Posted by Ebou's / Swahilivilla

No comments :

Post a Comment