Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi Yavuka Malengo, Wengi Wanaendelea Kumchangia...
2. Anonymous 500,000
3. Maggid Mjengwa 100,000
4. Raymond Kasoyaga 20,000
5.Edward Mgogo 10,000
6.Joachim Kiula 5,000
7.Libory Muhanga 5,000
8.Geofrey Kagaruki 10,000
9.Sadiki Mangesho 10,000
10. Edwin Namnauka 40,000
11.Daud Mbuba 10,000
12. Anonymous 200,000
13.Mikidadi Waziri 6,000
14. Bungaya Mayo 5,500
15. Abraham Siyovelwa 50,000
16. Godfrey Chongolo 22,222
17. Jacob Mwamwene 51,000
18. Denis Bwimbo 153,683
19. Zanzibar Ni Kwetu 150, 464
20.Felex Mpozemenya 10,000
21.Rweyendera Ngonge 11,000
22. Festo Temu 10,000
23. Azaria Mulinda 10,000
24.Khatibu Kolofete 5,000
25. John Bukuku 25,000
26. Abel 10,000
27. Hafidh Kido 10,000
28. George Mtandika 16,000
29. Shy-Rose Bhanji 200,000
30. Raymond Nkya 52,000
31. Maganga Sambo 10,000
32. Felix Mwakyembe 10,000
33. Abdul Diallo 5,000
34. Newton Kyando 20,000
35. Galanos Myinga 20,000
36. Anonymous ( 200 Euro) 497,000
37. Yasinta Ngonyani 50,000
38. Prosper/ Willy ( Japan) 314,000
39. Nuru Mkeremi 131,000
40. Anonymous 50,000
41. Josephine Mahimbo 50,000
42. Anonymous 150,000
43. Heladius Macha 30,000
44. Emma Malele 10,000
45. Anonymous 60,000
46. Hendry Mlay 35,000
47. Hosea Ngowi 10,000
48. Athuman Zuber 5,000
49. Hyancinth Komba 7,500
Jumla: 3,024,964 ( Milioni Tatu Na Ishir Na ini Na Mia Tisa Na Sitini Na Nne)
Lengo lilikuwa kukusanya 2,200,000 (Shilingi milioni mbili na laki mbili.) Hivyo, ndani ya saa 48 tumefanikiwa kufikisha na kuvuka lengo kwa shilingi 824,000 ( Laki nane na ishirini na nne elfu). Na michango zaidi bado inaendelea kutolewa. Mjengwablog itaendelea kupokea michango hiyo na kuikabidhi kwa mjane wa marehemu kama itakavyorekodiwa hapa. Hivyo, aliye dhamira ya kumsaidia mjane wa Marehemu bado anakaribishwa kutoa mchango wake. Siku ya mwisho ya kukusanya michango hiyo itakuwa Jumapili ijayo badala ya mwisho wa mwezi huu kama ilivyopangwa awali.)
Unaweza kuchangia kwa kutumia; M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa, Crdb A/ c 01j 2070759000 Maggid Mjengwa, NBC account ni 028201037642 jina Maggid Mjengwa. Tafashali nijulishe kama utatuma kwa njia ya Western Union au Benki)
Background:
Ndugu zangu,
Daud Mwangosi ambaye pia alikuwa ' Mwanakijiji' mwenzetu hapa Mjengwablog hatunaye tena.
Nimemfahamu Daud Mwangosi tangu mwaka 2004 nilipofika Iringa. Tangu wakati huo, amekuwa akiinipa ushirikiano mkubwa kwenye kazi ya kutangaza shughuli za kijamii kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi. Ni kwa kupiga picha za televisheni na kurusha habari kwenda Channel Ten; Iwe ni kwenda naye Ilula au Njombe, Daud Mwangosi alikuwa tayari kila nilipomwomba aongozane nami kwa shughuli ya kijamii.
Mara nyingi nilimkuta Daud ofisini kwake ( Picha ya kwanza juu) akichapa kazi na huku mkewe akimsaidia kazi nyingine. Daud Mwangosi alikuwa mbunifu. Alikuwa ni mwenye kiu ya kujifunza mambo mapya kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano.
Najua Daud Mwangosi alikuwa na malengo ya kuendeleza shughuli zake za ujasiriamali. Mbali ya mambo mengine, alikuwa na Photocopy machine ya kumwongezea kipato ambayo iliharibika mwaka jana. Akawa na ndoto ya kuwa na studio ndogo ya kupiga picha za vipande ( Passport Size). Yote ni katika kumwongezea kipato kutunza familia yake.
Leo Daud Mwangosi hayuko nasi. Ameacha familia, mjane na watoto wanne; Itika Mwangosi ( Mjane) Nehemia Mwangosi ( 17) Kidato cha Nne Malangali Sekondari, Hetzgovina Mwangosi (12) Bathsheba Mwangosi (9) na Moria Mwangosi ( 2)
Namini Daud Mwangosi angependa shughuli alizokuwa akizifanya ziendelee na zije kuwasaidia watoto wake pia.
Jana na leo nimewasiliana na mjane wa marehemu Mwangosi ambaye bado yuko Tukuyu. Nikamwambia kuna ' Wanakijiji ' wa Mjengwablog walioguswa na msiba wa Mwangosi na wangependa kutoa pole yao imsaidie katika kupata mwanzo kutoka hapa alipo sasa. Mjane wa Mwangosi amefarijika sana kusikia habari hizo.
Kwa vile tayari ameahidiwa msaada wa kusomeshewa watoto. Msaada anaouhitaji kwa sasa ni kupata photocopy machine ( Used) na kodi ya pango la ofisi. Jumla yake kwa yote hayo mawili haitazidi shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki mbili. Hivyo msaada anaouomba kwa wenye mapenzi mema ni shilingi 2, 200,000 ( Shilingi milioni mbili na laki mbili). Shughuli hizo zitamsaidia kujikimu.
Kutokana na hali aliyo nayo sasa, Mwenyekiti wenu napendekeza nichukue jukumu la kuratibu michango hiyo. Shime tushirikiane kufanikisha hili ili tumsitiri mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi.
Napendekeza ifikapo mwisho wa mwezi huu ( Septemba) tuwe tumefanikisha zoezi hili kwa yeyote aliye nacho, hata kama ni shilingi elfu tano, ni msaada mkubwa.
Mjengwablog bado tuna rekodi nzuri katika kuchangishana kuwasaidia wenye kuhitaji. Itakumbukwa, huko nyuma, kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya michango ile ya watoto wa Somalia na kuikabidhi UNICEF, Dar es Salaam. Ni zaidi ya shilingi milioni mbili.
Tulifanikisha mchango wa kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango, Madibira. Zaidi ya shilingi milioni nne.
Sasa ni zamu ya kumchangia mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Kinachohitajika ni milioni mbili na laki mbili.
Naam, kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.
Mwenyekiti wenu na familia yangu naanza kwa kuchangia shilingi laki moja.
Na kama kawaida, taarifa za waliochanga na kiasi kilichopatikana kitawekwa kwenye blogu kwa kila mmoja kuona.
Namna ya kuwasilisha michango: Tumia M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa)
Natanguliza Shukrani.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
No comments :
Post a Comment