Kaka Mjengwa: Usiwajali hao
wenye chuki binafsi!
wenye chuki binafsi!
- Tambua hutopendwa na wote!
- Wengi wetu tunakupenda na tunayatambua mema yako yote kwa jamii!
- Moja ya mema yako ni kuitisha ile Harambeeeeeeeeeee!
- Endelea kupata kombe la chai! (Tuna-assume kwenye kombe mnachai na sio........)
/Geo Kimbi
Ndugu zangu,
Jana nzima nilikuwa kibaruani . Usiku nikaingia kule kwenye jukwaa la JF. Nikapitia comments zote kwenye thread yangu nilyoingiza asubuhi ya Jumapili ya jana. Ilihusu nilichokiona na kukisikia kule kijijini Nyololo. Kuna waliotoa maoni yaliyojaa chuki na mashambulizi binafsi, mpaka unashangaa.
Ukweli, kuna wanaonekana kuandika maoni yao yaliyojaa chuki badala ya hoja. Wakati mwingine najiuliza; hivi hawa ni Watanzania? Maana, Watanzania hatuna hulka ya chuki za namna hii. Kuna mwingine akiliona jina langu tu anatanguliza chuki. Na kila sentesi yangu niliyoandika anatafuta ni wapi nimeteleza ili anishambulie. Kuna ambao hawaoni hata moja jema la kwangu.
Inanikumbusha kisa cha Idi Amin na mwandishi wa Kitanzania.
Inasemekama makachero wa Idi Amin walimnasa mwandishi wa Kitanzania ndani ya mpaka wa Uganda. Mwandishi yule akafikishwa mpaka kwa Idi Amin mwenyewe.
Alipofika kwa Amin, mwandishi yule wa Kitanzania akaamini kuwa amekwisha, kuwa atauawa. Idi Amin akamkaribisha kiti na soda anywe. Kisha akamwuliza; " Hivi nyinyi waandishi wa Tanzania mnaandika mabaya tu kuhusu mimi. Nikuulize, unadhani hakuna hata jambo moja zuri ambalo Idi Amin amelifanya?"
Mwandishi yule Mtanzania akajibu; " Ni mengi tu mazuri umefanya Mheshimiwa Rais!"
Idi Amin akatamka; " Kama ni hivyo, basi, rudi nyumbani Tanzania nenda ukaandike jambo moja tu zuri kuhusu Idi Amin!"
Mwandishi yule Mtanzania hakuamini masikio yake kuwa Idi Amin amemwachia huru!
Usiku Mwema.
Maggid,
Iringa.
0788 111 765
...Nje ya Mada Kidoogo. Nadhani sub-headline ya Blog yako inapaswa kuwa:
ReplyDelete'This Blog is ABOUT Zanzibar and Tanzania as a Whole'.
Na sio:
'This Blog is ON Zanzibar and Tanzania as a Whole'.