Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharifu Hamadi Amewahakikishia Uongozi wa Zanzibar Diaspora Asociation(ZADIA) kuwa Serikali imeanzisha Kitengo maalum katika Ofisi ya Rais wa Zanzibar kwa ajili ya kushughulikia na kuendeleza Ushirikiano na wazanzibari walioko nje kwa manufaa yao.
Maalim Seif Aliyasema hayo jana Wakati alipokutana na Uongozi wa ZADIA katika Marriott Hotel Washington D.C.
Amesema hivi sasa Serikali Inaitambua Zanzibar Dispaora Asociatin Kisheria hivyo amewahakikishia kufanya kazi zao bila ya hofu ili kuisaidia zanzibar.
Aidha Makamo wa Rais Aliwasihi Uongozi huo kutumia Ujuzi wao walioupata nje kwa manufaa ya Zanzibar na kuwataka kupata idadi ya wazanzibari walioko hapa Marekani pamoja na Uzoefu na Elimu zao ili wakienda likizo Nyumbani waweze kutoa Ushauri wao kwa jamii kwa kushiriana na Serikali.
Mapema Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Asociation Bwana Omari Ali amemueleza Maalim Seif kuwa wanahitaji Ushirikiano na nyenzo kutoka nyumbani ili waweze kupiga hatua mbele.
Hata hivyo Alisema Zanzibar Diaspora ina wataalam wenye Ujuzi wa fani mbali mbali ambao wataweza kuisaidia Zanzibar katika nyanja ya Elimu,Utafiti na Kiufundi ili zanzibar ipige hatua zaidi ya maendeleo.
Alimueleza pia Diaspora yao Iliaza na watu wachache na kuwataja Dk Moh'd Adam aliopo Pennsylvania,Dk Hassan Omar Ali (Texas), Dk Halfani aliopo Indiana, Amir Ali Washington seattle, Haji Jingo Califonia,na Dk Alawia Omar alioko Indiana.
Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Asociation Bwana Omari Ali (Picha ya juu) na bwana Shamis Abdullah Katibu wa Zanzibar Diaspora (chini)
Maalim aliwaeleza pia alikuja Marekani kwa Mwaliko wa Chama cha Rais Obama kwa kupitia taasisis Ya NDI kwenye convention ya Rais Obama huko North Carolina. (Picha zote na swahilivilla.blog)
Source: Swahilivilla
No comments :
Post a Comment