REST IN PEACE BROTHER!
DAUD MWANGOSI
Wagagagigikoko News Network (WANENE) inaungana na Wana-habari wote katika kuomboleza kifo cha ndugu yetu Daud Mwangosi kilichotokea kwenye mikono ya vyombo vya usalama nchini.
Blog la ZANZIBAR NI KWETU ambacho ni chombo cha WANENE kinaomboleza mpaka tarehe 10 September, 2012. Katika wakati huu wa kuomboleza hatutotoa habari zozote kuhusu vyombo vya usalama nchini, kwani vyombo vyetu vya usalama nchini vimegeuka kuwa sawa na vyombo vya usalama vya enzi za ukoloni.
Kwa upande mwengine kifo cha Mwangosi kiwe somo na fundisho kwa Wazanzibari wote wanaotaka kujigomboa. Ikiwa wameweza kumuuwa Mtanganyika mwenziwao kinyama kama ilivyotokea, je Mzanzibari atafanywa nini? Atauliwa kama kuku! Ni lazima tujihadhari na hawa majangiri!
Mola awalani wote wenye damu ya Mwangosi kwenye mikono yao.
MOLA AMLAZE MTANZANIA MWENZETU
PEMA PEPONI. AMEN!
PEMA PEPONI. AMEN!
Picha na Mjengwa
No comments :
Post a Comment