Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 26, 2012

GNU IMETAKIWA KUIGA MFUMO WA KIISLAMU KATIKA UENDESHAJI WAKE..


Dr Ali Shein - Rais wa Zanzibar 
Written by   //  26/10/2012  //  Habari  //  No comments
Dr Shein pamoja na viongozi wenzake wa serikali ya umoja wa kitaifa wametakiwa kuiga mfano wa uongozi wa Mtume Muhammad S.A.W katika kuendesha serikali ya Zanzibar ili kuweza kulinda haki za raia na kuleta uadilifu katika jamii.
Hayo yameelezwa na ust Haji F arouq katika msikiti wa Biziredi mwembeladu zanzibar alipokua akiwahutubia waumini wa dini ya kiislamu katika hotuba ya sala ya Ijumaa..
Ameelezea kusikitishwa na tamko la serikali na baadhi ya viongozi wa dini  wa kiserikali kutamka wazi kwamba wamechoshwa na vitendo vya uamsho, amesema hawakupaswa kusema hayo bali walitakiwa kuwasikiliza wananchi hao na kukaa pamoja kwa nia safi ili kuweza kutafuta njia sahihi ya kuweza kutatua migogoro ambayo inatokea zanzibar.
Amesema vitendo vyote vilivyotokea zanzibar ambavyo vinadaiwa kuwa  wananchi ndio wamevisababisha bado havijafikia ukubwa wa kuwa serikali ilipe kisasi kwa wananchi kwa kuwapiga na kuwapa kesi za kuwazushia pamoja na kuwafanya waishi wakiwa na hofu kubwa kwani mambo haya yanaweza yakasababisha kusambaratika kwa umoja wa wazanzibar. Hivyo amemtaka rais wa zanzibar na wasaidizi wake wamuangalie mtume s.a.w amefanyiwa nini  na makafiri lakin hakulipa kisasi bali yeye alikua akiwafanyia ukarimu,.
Akisoma baadhi ya aya za qur-an na hadiithi za mtume S.A.W  katika kutilia mkazo mada yake amesema waislamu wanatakiwa waheshimiane kwa heshma ya dini yao, vile vile uislamu unatufundisha kuwatunza na kuwaheshimu wanazuoni ambao elimu zao wanazitumia kuwafundisha wenziwao na sio kukaa ukajiita wewe mwanazuoni kwa kusoma nchi za nje halafu usiitumie elimu yako, hivyo amesema kitendo cha kuwanyima dhamana viongozi wa uamsho ambao ni miongoni mwa wanazuoni wanaotoa mchango mkubwa katika kuipeleka mbele dini ya kiislamu zanzibar ni kuwadhalilisha na kuwatukana mashehe.
Akimalizia hotuba yake amesema waislamu wanapaswa kuwa na umoja na kuonesha kuchukizwa iwapo muislamu atahujumiwa au kufanyiwa kitendo ambacho si kizuri kufanyiwa muislamu hivyo amewatahadharisha waumini wa kiislamu kuepuka kuwa kama baadhi ya waislamu ambao wamefurahishwa na kitendo cha serikali kuwadhalilisha raia na baadhi ya viongozi wa dini ambao wanaelezea mambo ya serikali yaliyojificha kwa maslahi ya taifa…..
Chanzo: Mzalendo


No comments :

Post a Comment