Written by Stonetown (Kiongozi) // 26/10/2012
IDD MUBARAK WA KULLU AAM
WAANTUM BIKHEIR
Kwa Niaba ya Jumuiya ya Zanzibar Welfare Association UK, nawatakia waislamu wote duniani siku kuu ya kheri na baraka.
Tunamuomba Mola wetu mlezi awarehemu wazee wetu wote waliotangulia mbele ya haki na awasamehe makosa yao.
“sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake vyote vilivyomo Mbinguni na Ardhini. Na Akhera, sifa njema ni zake pia; Naye ni Mwenye Hekima na Mwenye Ujuzi wa kila jambo”.
Kwa utukufu wako huo tunakuomba Allah tuondolee madhila, maradhi na kila lililobaya kwetu waja wako wote, tutie imani ya kukutumikia wewe na utupe mwisho mwema hapa duniani na utufunike na rehma zako kesho akhera ili tuwe wenye kufuzu.
Mola wetu wakubalie mahujaji wote hijja zao ziwe mabruur, na uwape uwezo wa kufanya ibada hii ya hijja kila ambae hajakuwa na uwezo wa kufanya ibada hii tukufu.
Mola wetu wewe ndie tunaekuabudu na ndie tunaekuomba msaada.
No comments :
Post a Comment