Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 19, 2012

KAMISHNA AZUNGUMZA ZANZIBAR!


 Kamishna wa Polisi Mussa Ali Mussa akifafanua jambo katika Mkutano na Waandishi wa Habari akielezea juu ya Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo umefanyika hapo katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika Mkutano wa Jeshi la Polisi kuelezea juu ya Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo umefanyika hapo katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.

Salma Said, Zanzibar

ASKARI Mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), CPL Said Abdulrahman amepigwa mapanga na watu wanaosaidikiwa kuwa ni wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) jana usiku katika eneo la Bububu kufuatia vurugu zilizoanza juzi hapa nchini.


Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa huko ofisini kwake Ziwani Mjini Unguja alisema kumetokea tukio la kusikitisha lililosababishwa na fujo zilizotokea ambazo zinatokana na Jumuiya ya Uamsho ambapo polisi huyo aliuwawa kinyama kwa askari huyo mwenye namba F.2105 ambaye anatoka kikosi cha FFU Mkoa wa Mjini Magharibi.

“Wafuasi wa Uamsho wamempiga mapanga kichwani na mikononi wakati akirudi kazini majira ya saa 6:30 za usiku eneo la Bububu. Tuelewe kwamba aliyeuliwa ni askari polisi, ni raia wa Tanzania na ni muumini wa dini ni lazima tuhakikishe waliofanya unyama huu wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kama sheria za nchi zinavyotuelekeza” alithibitisha Kamishna huyo.
Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa kiongozi wa Taasisi za Kiislamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed katika mazingira ya kutatanisha Kamishna alisema majiraya saa 6:30 mchana wa juzi kituo cha polisi walipokea taarifa kutoka kwa Sheikh Msellem Ally kwamba kiongozi mwenzao wa Jumuiya ya Uamsho ametekwa na haonekani tokea jioni ya Octoba 16 mwaka huu.

“Baada ya taarifa hii uchunguzi ilianza na mmoja wa watu waliohojiwa ni Said Omar Said ambaye ni ndugu wa Sheikh Farid ambaye ni dereva na ndiye aliyekuwa naye walipokwenda katika eneo la Mazizini kununua umeme kutokana na maelezo ya dereva huyo” alisema Kamishna Mussa.

Kamishna Mussa alisema kwa mujibu wa Said kwamba Sheikh Farid alimuamuru dereva huyo kwenda nyumbani kupeleka umeme wakati yeye akizungumza na watu aliowaita ambapo wakati huo walikuwemo ndani ya gari ya NOAH ambayo nambari zake hazijajuliana ambapo dereva huyo aliporudi nyumbani hakumkuta tena Sheikh Farid eneo alilomuacha na wageni wake.

Alisema majira ya saa 6:30 juzi wakati taarifa hizo zinapelekwa kituoni huku wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho walijikusanya katika msikiti wa Mbuyuni na kuanzisha fujo kwa kuanza kuchoma moto kwenye jaa la karibu na msikiti huo ambapo baadae fujo hizo zikasambaa katika maeneo mengine ya Mjini kwa kufanyika uharibifu wa mali za Serikali, Chama Cha Mapinduzi na wananchi wa kawaida.

“Mbali ya khofu kubwa kwa wananchi juu ya maisha na mali zao, fujo hizi zilileta hasiraya kuchoma na kuharibu miundombinu ya barabara, kuharibu maskani za chama tawala CCM za Kisonge Muembeladu kwa kuchoma moto gari moja ya serikali ilivunjwa kioo kidogo cha pembeni, gari ya zimamoto kuvunjwa kioo cha mbele pamoja kuvunja duka la pombe na kuiba mali zilizokuwemo ndani” alisema Kamishna huyo.

Aidha Kamishna Mussa amesema hadi sasa jumla ya watu kumi wameshakamatwa na wapo mikononi mwa polisi kwa tuhuma za makosa mbali mbali yaliotokea juzi katika vurugu hizo, na upepelezi wa kujua ukweli juu ya uvumi wa kutekwa kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed bado unaendelea huku misako mbali mbali ikiwa imeanzishwa kuwakamata wale wote waliofanya mauaji na vitendo vya kihalifu vya kuharibu mali za watu na miundombinu ya barabara.

Akiwatoa khofu wananchi juu ya hali ya usalama Kamishna Mussa alisema hali ya Mji wa Zanzibar kwa sasa ni shwari wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida ambapo jeshi la polisi kwa kushirikiana na vikosi vyengine vya ulinzi na usalama viteendelea kuhakikisha amani inadumu muda wote.

“Polisi tunawahakikishia wananchi wote kuendelea kuwa wastahamilivu na tutaendelea kuitii na kuilinda serikali iliyopo madarakani. Tunaendelea kuwaomba wananchi kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao, kutupa taarifa za watu waliohusika na vurugu pamoja na mauaji ya askari wetu. Tuendelee kukumbushana kutii sheria bila ya shuruti” alimalizia kusema Kamishna huyo.

Source: Vijimambo

No comments :

Post a Comment