Tanzania, Malawi sasa kurejea mazungumzo
Rais wa Malawi, Joyce Banda
Thursday, October 18, 2012
Serikali ya Malawi imekubali kurudi katika meza ya mazungumzo kuhusu mgogoro wa
mpaka katika Ziwa Nyasa kati yake na Tanzania.
Malawi imechukua uamuzi huo baada ya hivi karibuni Rais wa nchi hiyo, Joyce Banda,
kutangaza kujiondoa katika mazungumzo hayo.
Hatua ya kuendelea kwa mazungumzo hayo ilitangazwa jana na Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule, wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Haule alieleza uamuzi huo baada ya waandishi wa habari waliohudhuria
uzinduzi wa Wiki ya Umoja wa Mataifa kumuuliza kuhusu hatma ya
mgogoro huo kati ya nchi hizo mbili baada ya Malawi kujiondoa katika
mazungumzo na kutaka kulipeleka suala hilo katika Mahakama ya kimataifa
ya Uusuluhishi wa Migogoro (ICJ).
Akijibu alisema: “Kuhusu swali ulilouliza, wenzetu wa Malawi watakuja nchini
kuanzia tarehe 27, Oktoba.”
Alisema baada ya ujumbe wa Malawi kuwasili nchini, vikao vya mazungumzo
kuhusu mgogoro huo wa mpaka wa Ziwa Nyasa vitaanza.
Hata hivyo, Haule hakulitolea ufafanuzi zaidi suala la mazungumzo ya kusaka
amani katika mzozo wa mpaka huo ambao katika miezi ya karibuni,
ulisababisha kuzorota kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili, ambazo ni
wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).
Mwezi uliopita, Rais wa Malawi, Joyce Banda, muda mfupi baada ya kuwasili
nchini humo akitokea New York, Marekani alikokutana na kufanya
mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon,
alitangaza nchi yake kujitoa katika meza ya mazungumzo kuhusu mgogoro
huo wa mpaka katika Ziwa Nyasa na kutangaza kuupeleka ICJ.
Kwa mujibu wa Banda, serikali yake iliamua kuchukua hatua hiyo kwa madai
kuwa Tanzania imevuruga makubaliano yaliyofikiwa nchini humo ya kuendelea
katika meza ya mazungumzo baada ya kuchora ramani mpya inayoonyesha
kuwa mpaka unapita katikati ya Ziwa Nyasa, kuweka bendera katika eneo l
enye mzozo na wavuvi wa Malawi kunyanyaswa.
Kabla ya kwenda New York, Rais Banda, alikutana na Rais Jakaya Kikwete,
mjini Maputo Agosti 17, mwaka huu na kufanya mazungumzo, ambayo
yalimridhisha Rais Banda kwamba mgogoro huo wa mpaka hauwezi
kusababisha vita kati ya Tanzania na Malawi.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika wakati wa mkutano wa wakuu
wa nchi na serikali wa Sadc, Rais Kikwete alisema kuwa Tanzania haina
mpango wowote wa kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Malawi.
Alisema kuwa yeye akiwa Amiri Jeshi Mkuu, hajawahi kuwa na wazo la
kutumia nguvu za kijeshi katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wa Tanzania, Bernard Membe, alisema mahakama hiyo isingeweza kusuluhisha mgogoro huo kwa kuwa Tanzania haijasaini mkataba wa kuanzishwa kwake.
Rais Kikwete alipokutana na Ban Ki-moon mjini New York mwezi uliopita,
alipongezwa kwa kutumia mazungumzo katika kumaliza mgogoro wa
Ziwa Nyasa.
Mgogoro huo unatokana na Tanzania kusema kuwa kila nchi inamiliki
mpaka wa Ziwa Nyasa kwa asilimia 50 wakati Malawi ikisema inalimiliki
kwa asilimia 100.
Mazungumzo ya awali, yaliwashirikisha mawaziri na wataalam kabla ya
Malawi kujitoa yalifanyika Dar es Salaam na Muzuzu.

CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment