Mawakili wametishia kujitoa katika kesi hyo kwa madai ya usumbufu wanaoupata wateja wao. Mawakili hao ni Salim Tawfik na Abdallah Juma wanaowawakilisha Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake sita. Leo hii wamesusa kabisa kuingia mahakamani na wamesema wanakusudia kujitoa kutokana na uusmbufu wanaofanyiwa wateja wao wa kuhawangaisha.
Na sasa hivi mawakili hao wameshaondoka na watuhumiwa ndio wanafikishwa mahakamani wakiwa wamenyolewa ndevu zote wakiwa mahabusu. Kesi leo inatarajiwa kutolewa maamuzi ya masharti ya dhamana yaliyokuwa yanapingwa na mawakili wa utetezi ambao wameshaondoka mahakamani hapa.
Hatujui nini kitaendelea tena maana watu wamezuiliwa kuingia katika eneo la mahakamani.
Sheikh Farid akiwa kanyolewa ndevu akiwasili mahakama ya Vuga leo.
MORE UPDATES:
Sheikh Farid na wenzake wasomewa mashtaka mapya:
1) Kusababisha uvinjifu wa amani zanziba
2) Kusababisha uharibifu wa mali kisiwani zanzibar kutokana na vurugu
3) Kushawishi na kuchochea vurugu zilizosababisha kuhatarisha maisha ya watu na serikali kuingia hasaraK
1) Kusababisha uvinjifu wa amani zanziba
2) Kusababisha uharibifu wa mali kisiwani zanzibar kutokana na vurugu
3) Kushawishi na kuchochea vurugu zilizosababisha kuhatarisha maisha ya watu na serikali kuingia hasaraK
Aidha mtuhumiwa mmoja anatuhumiwa kumtukana Kamishna wa Polisi Zanzibar Musa Ally Musa
washtakiwa wote wamenyimwa dhamana kwani ni Jaji pekee ndie anayeweza kutoa dhamana kwa makosa yao lakini wana haki ya kukata rufaa kudai dhamana katika mahakama ya juu.
Chanzo: Jamii forums
No comments :
Post a Comment