Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 23, 2012

MAALIM SEIF ASEMA:

"KUTOKUWEPO KWA MIKAKATI IMARA YAKUENDESHA NCHI NDIO CHANZO CHA MIGOGORO"

Maalim Seif Shariff Hamad
Written by   //  23/10/2012 
Katibu mkuu wa chama cha wananchi cuf maalim seif sharif Hamad amedai kuwa chanzo kikuu cha migogoro ya kijamii ikiwemo ya ardhi na mizozo ya kidini inatokana na kutokuwepo kwa mikakati imara ya kuendesha nchi, na kwamba viongozi wanapaswa kujifunza kutokana na migogoro hiyo, ili kuweka mikakati imara ya kuendesha nchi kwa uhakika.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Buguruni jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa chama hicho kwenye mkutano maalum wa hadhara uliolenga kuwakaribisha wanachama wapya na kuwapokea wanachama walioamua kurejea CUF baada ya kukihama na kuhamia vyama vyengine.
Aidha Maalim Seif amesema kuwa Tanzania imekuwa ikipita katika kipindi kigumu cha migogoro na uvunjifu wa amani, mambo ambayo yanapaswa kupigwa vita ili kurejesha hali ya amani na kuvumiliana.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa chama chake kitaendelea kutetea na kutekeleza sera yake ya kuwaunganisha watanzania popote walipo bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Amesema operesheni mchakamchaka hadi mwaka 2015 iliyozinduliwa na chama hicho hivi karibuni imekuwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo, na kwamba tayari imeanza kuleta mafanikio katika mikoa iliyoanza kutekelezwa ukiwemo mkoa wa Arusha.
Katika mkutano huo Maalim Seif aliwapokea na kuwapa kadi za chama hicho wanachama kadhaa walioamua kurejea chama hicho wakitokea chama cha ADC wakiongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa ADC Bw. Al-Badawi.
Kabla ya kujiunga na ADC, Bw. Al-Badawi alikuwa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Temeke, na sasa ameamua kurejea CUF kwa kile alichokieleza kuwa ni ubabaishaji ndani ya chama hicho kipya kinachohusishwa na mbunge wa jimbo la Wawi Mhe. Hamad Rashid Mohd.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment