Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 17, 2012

MAALIM SEIF AUNGURUMA NUNGWI!

MAALIM SEIF AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA NUNGWI



Wanachama, wapenzi na wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CUF alipokuwa 
akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara Nungwi

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad 
amesema  mamlaka kamili ya Zanzibar yatapatikana kwa kila Mzanzibari 
kuhakikisha anaweka mbele mapenzi yake kwa nchi yake na kuweka kando
itikadi ya chama chake cha siasa.
Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara huko Nungwi, mwishoni mwa wiki 
iliyopita, Maalim Seif alisema vyama vya siasa huanzishwa na baadaye 
kuondoka, lakini Zanzibar itaendelea kuwepo, hivyo Wazanzibari wote waone 
ni jukumu lao kuhakikisha ni yenye mamlaka kamili iliyostawi kiuchumi na 
maendeleo ya watu wake.
“Tulikuwa na ASP, Hizbu, Umma Party, ZPPP na vyenginevyo, leo vipo... Zanzibar
ipo haipo? Zanzibar imekuwepo hata kabla ya Tanganyika, Uganda na Kenya 
na Inshaallah itaendelea kuwepo mpaka kiyama” alieleza.


Alisema hakuna mtu anayechukia Muungano, lakini ni ukweli ulio wazi kwamba 
Muungano wetu ni wa ‘Mkubwa na Mdogo’, hali ambayo matokeo yake 
ni kila siku zinavyokwenda mbele Zanzibar ndiyo inayoathirika zaidi katika nyanja 
tafauti.


“Mimi ni mwanachama wa CUF, ni muasisi wa CUF, naipenda sana CUF, lakini 
ukinipasua moyoni damu yangu itajiandika ‘Zanzibar’. Sote tunatakiwa tuwe 
Wazalendo wa Zanzibar, nchi kwanza vyama baadaye”, alisema Maalim Seif.


Maalim Seif alisema baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaodai Muungano huu 
uliopo sasa ni mzuri inawezekana wanasema hivyo kwa sababu wananufaika wao 
binafsi, lakini Muungano huo tokea mwaka 1964 umekuwa na matatizo mengi 
na makubwa, ambayo matokeo yake ni kuzorotesha uchumi na hadhi ya Zanzibar.


Alisema juhudi kubwa zimechukuliwa kutatua kasoro zilizopo na sasa ni zaidi 
ya miaka 48, lakini kama kwamba zimezidi kuongezeka, na kuhimiza wakati ndio 
huu wananchi wa Zanzibar kuweka kando itikadi zao za vyama vya siasa na 
kuhakikisha wanapata mfumo wa Muungano ambao hautaibana Zanzibar katika 
kujiamulia mambo yake kwa namna yoyote ile.

Kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara huko katika viwanja vya Nungwi Sokoni, 
Maalim Seif alikagua miradi ya barabara za ndani katika jimbo la Nungwi 
zilizojengwa na viongozi wa jimbo hilo, wakiongozwa na Mwakilishi wa Nungwi, 
Haji Mwadini Makame na Mbunge Yussuf Haji Khamis.

Pia alikabidhi vifaa mbali mbali, vikiwemo kwa ajili ya miradi ya maji safi na salama 
katika vijiji vilivyopo ndani ya jimbo hilo pamoja na kukabidhi kadi kwa 
wanachama wapya waliojiunga na chama cha CUF.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alisifu 
juhudi kubwa zinazoendelea kuchukuliwa na viongozi wa jimbo la Nungwi kwa 
mashirikiano na wananchi, na kuzielezea hatua hizo kuwa ni mfano wa kuigwa 
na viongozi wa wananchi katika maeneo mengine.

“Viongozi wa jimbo hili wanatekeleza kikamilifu sera za Chama cha 
Wananchi CUF za kuwaondolea shida wananchi, ni imani yangu kuwa 
iwapo watapata mashirikiano mazuri kutoka Wilayani, Mkoani na Halmashauri 
watafanya mambo makubwa zaidi na matatizo mengi ya wananchi wa Nungwi 
yataondoka kabisa”, alisema Makamu wa Kwanza wa Rais.

Mapema wananchi wa kijiji cha Mvuleni jimboni humo, walimueleza Makamu wa 
Kwanza wa Rais kuwa wamefarajika sana kupata barabara hiyo inayokwenda hadi 
kijijini kwao, kwa sababu kwa muda wote tokea kuwepo kijiji hicho walikabiliwa na 
shida kubwa ya usafiri, ikiwemo pale inapotokea haja ya kuwawahisha wagonjwa 
kupatiwa matibabu

No comments :

Post a Comment