Maalim Seif Sharrif Hamad
Sunday, October 28, 2012.
“Malengo ya Dira ya Mabadiliko ni kuwaelewesha… Matumizi sahihi ya utajiri wa rasilimali za asili katika nchi yetu, uboreshaji wa huduma za msingi za kijamii ikiwa ni elimu, afya, na miundombinu, Mikakati ya CUF juu ya kuimarisha uchumi wa Taifa na kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi,” alisema.
CHAMA Cha Wananchi CUF leo kinatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara mjini Morogoro ikiwa ni muendelezo wa operesheni zake za kukiimarisha chama hicho.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho Taifa kupitia Mkoa wa Morogoro, Mbarala Maharagande alisema jana kuwa mkutano huo unatarajiwa kuhutubiwa na katibu mkuu wake wa taifa, Maalim Seif Sharif Hamad.
Maharagande alisema pamoja mambo mengine, maalim Seif katika mkutano huo, atapata fursa ya kuzungumzia hali ya kisiasa nchini na ufafanuzi wa falsafa ya chama hicho ya ‘Dira ya Mabadiliko’.
Maharagande alisema pamoja mambo mengine, maalim Seif katika mkutano huo, atapata fursa ya kuzungumzia hali ya kisiasa nchini na ufafanuzi wa falsafa ya chama hicho ya ‘Dira ya Mabadiliko’.
Alisema CUF kimekuwa katika mpango wa kuzungumza na wanachama wake nchi nzima na kutumia falsafa hiyo ya Dira ya Mabadiliko inayosisitiza juu ya Amani na Maendeleo ya watu na nchi yao.
“Malengo ya Dira ya Mabadiliko ni kuwaelewesha… Matumizi sahihi ya utajiri wa rasilimali za asili katika nchi yetu, uboreshaji wa huduma za msingi za kijamii ikiwa ni elimu, afya, na miundombinu, Mikakati ya CUF juu ya kuimarisha uchumi wa Taifa na kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi,” alisema.
Alisema Maalim Seif pia anatarajia kuhudhuria mkutano wa hadhara wa chama hicho katika Wilaya ya Mvomero-Kata ya Mtibwa kwa ajili ya kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.
Maharagande aliwataka wapenzi na wafuasi wa chama hicho Wilaya ya Morogoro Mjini kujitokeza kwa wingi kumpokea katibu mkuu ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais katika serikali ya umoja wa kitaifa.
Chanzo: Mwananchi
No comments :
Post a Comment