Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 30, 2012

‘Mmemchukua yuhai mnamrejesha maiti?’ Baba wa Hamad

Mzee Ali Kaimu ni baba wa kijana Hamad ambaye alikamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama lakini akafariki katika mikono yake ikidaiwa baada ya kupata kipigo kikubwa na kusababisha kifo chake
October 29, 2012.

Kijana mmoja makazi wa Magomeni Unguja Hamad Ali Kaimu (20) anadaiwa kufariki dunia akiwa mikononi mwa jeshi la polisi baada ya kupigwa hadi kufa katika operesheni za kuwasaka wahalifu na wenye kusababisha vurugu Zanzibar.
Zoezi hilo limekuja kufuatia kutokea uvunjivu wa amani na uharibifu wa mali na miundombinu baada ya kudaiwa kutoweka kwa kiongozi wa taasisi za Kiislamu Sheikh Farid Hadi Ahmed  Otoba 16, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari hizi baba mzazi wa kijana huyo Mzee Ali Kaimu amesema mwanawe aliondoka nyumbani kwenda kufungua ngombe hivyo alikutana na askari hao wakiwa kazini na kumchukua na alipomfuata mwanawe nao alipata kipigo kutoka kwa polisi hao ambao wakiwa na wenziwao wa vikosi vya SMZ.
Mwanangu aliniomba shilingi 30,000 kwa ajili ya kununulia godoro na yeye mwenyewe alikuwa ni 20,000 kwa hivyo alikuw ana jumla ya shiligi 50,00 ili akanunue gorogo lakini alipokamatwa nikajua wale askari watazichukua wao zile pesa na hawatazifikisha kituoni kwa hivyo mimi nikazifauata ili anipe kwa kuwa aliniita baba njoo uchukue huu mzigo na nilipofika polisi wakanipiga kweli kweli” alisimuliza baba huyo.
Marehemu Hamad alikamatwa na jeshi la polisi Octoba 26 mwaka huu majira ya saa 11 jioni na kufariki majira ya saa moja usiku akiwa mikoni kwa polisi na kusababisha malalamiko makubwa kutoka kwa familia yake.
Zaidi ya wananchi hamsini leo walikutana na waandishi wa habari na kutoa kilio chao wakilalamikia vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika utelelezaji wa zoezi hilo ambapo kijana mmoja Hamad Ali Kaimu alifariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa na vikosi hivyo vya usalama katika zoezi hilo.
Miongoni mwa waliozungumza na waandishi ni baba mzazi wa kijana huyo, Ali Kaimu mkazi wa Nyerere ambaye alidai mtoto wake alipigwa hadi kufa akiwa mikononi mwa jeshi la polisi  Oktoba 27 na kuahidi kutokubali kuacha kitendo hicho kiikapita bila ya kuchukua hatua za ksiheria za kwenda mahakamani.
Kwa mujibu wa baba huyo aliomuona mtoto wake akiitwa na polisi wakati akenda kufunga ngombe na kuanza kupigwa akiwa mbele ya macho yake na alipokwenda na yeye alipigwa.
Alinita mwanangu baba njoo uchukue mzigo wangu na nikuoneshe nilipomfunga ngombe wangu na nilipokwenda polisi na mie wakaniangushia kipigo kikali sana na mwanangu alikuwa na shilingi 50,000 za kununulia godoro sasa alitaka kubnipa lakini walikataa anikabidhi” alisema baba huyo kwa huzuni.
Kwa mujibu wa taarifa za baba wa Marehemu Hamad mwenye umri wa miaka 22 alisema kijana wake alikamatwa na polisi siku ya sikukuu na kupigwa wakati akiwa katika shughuli za kulisha ng’ombe huko Magomeni.
Akiendelea kusimulia mkasa huo Kaimu alisema siku ya pili alipigiwa simu akiitwa katika kituo cha polisi cha Madema na alipokwenda akatakiwa kwenda hospitali ya Mnazi Mmoja kuchukua maiti.
Walinipigia simu nikachukue maiti yangu na mimi nikagoman kwa sababu wamemchukua mwanangu akiwa hai na nikawaambia munikabidhi mwanagu akiwa hai kwa sababu hawajamchukua maiti sasa vipi watanipa mwanangu maiti?” alihoji Mzee huyo.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alikiri kuwepo kwa operesheni ya kamatakamata lakini amekanusha polisi wake kuhusika na kitendo cha kumkamata na kumpiga kijana hiyo hadi kufa.
Kamishna Mussa alisema jeshi la polisi lilikwenda kumuokoa kijana huyo baada ya kuzungukwa na watu katika eneo la Magomeni alionekana akipigwa huku akisisitiza kwamba kumbukumbu za polisi zinaonyesha kijana huyo alikuwa ni mwizi mzoefu.
Wananchi wengine wakiongea mbele ya waandishi walisema wamechoshwa na vitendo wanavyofanyiwa na jeshi la polisi kwa kushirikaina na vikosi vya SMZ kwa kuwapiga, kuwapora mali zao na kuwafanyia unyanyasaji na udhalilishaji mbele ya familia zao katika majumba kwa kisingizio cha kutafuta wahalifu.
Tunasema tumechoshwa na vitendo hivi maana tunajua kuwa sisi kujitokeza mbele ya waandishi tutakuja kupigwa tena tukionekana hizi sura zetu lakini tunasema tumechoshwa na udhalilishaji huu ..na tunaiomba serikali itusaidie jamani” alisema Mama mmoja huku akiangusha kilio.
Akisimulia mkasa uliomkuta ndani ya nyumba yake alisema amepigwa sana yeye na mume wake huku watoto wake wakimwagiwa maji bila ya sababu yoyote na walipohoji wakatakwia kunyamaza kimya na kutishiwa kupigwa risasi iwapo wataendelea kuhoji.
Tukawa tunahoji kwani tmefanya kosa gani sisi? Wakatwambia nyamazeni kimya tutakupigeni risasi sasa hivi wajinga wakubwa” hivyo ndivyo alivyosema maam huyo ambaye hawakupenda kutajwa majina yao kwa ajili ya usalama wao.
Katika hatua nyengine  Chama  Cha Wananchi (CUF) kimelaani vitendo vinavyofanywa na jeshi la polisi kwa kukiuka haki za msingi za raia na kuitaka serikali kusitisha mara moja udhalilishaji huo wa wananchi.
Hatukatai kuendeshwa kwa operesheni za kuwasaka wahalifu sisi tunaunga mkono waliotenda makosa wafikishwe katika mikono ya sheria lakini tujiulize jee kumkamata mtu ukampiga, ukamuadhibu na kumtesa na hata kumuuwa ndio unaondosha tatizo au unazidisha tatizo” alisema Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Salim Bimani
Alisema serikali lazima itekeleze wajibu wake kwa raia zake bila ya kuwanyanyasa kwani vitendo vinavyofanyika sasa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za raia ndnai ya nchi yao huku akisiistiza kwamba wenye kuathirika zaidi ni wafausi wa chama chao.
Bimani aliwaambia waandishi wa habari kwamba serikali na vyombo vyake vya dola vifanyekazi bila kuwahujumu na kuwasumbua wananchi wasiokuwa na hatia kwani kuendelea kuwaadhibvu wananchi ni kwenda kinyume na utawala wa sheria ambao Tanzania inajivunia kuheshimu haki za binaadamu.
Alisema utekelezaji wa operesheni hiyo na vitendo vya hujuma vinaiweka Zanzibar katika machafuko wakati wananchi wamekuwa watulivu licha yakuwepo hali tete ya kisiasa visiwani humo.
Aidha alisema chama chake kinalaani mauaji yaliofanywa na watu wasiojulikana ya Koplo Said Abdulrahman na kinalaani machafuko yote yaliotokea nchini na kulitaka jeshi la polisi kutimiza wajibu wake wa kuwakamata wahalifu na wenye makosa bila ya kukiuka taratibu za kisheria.
CUF kinalaani vitendo hivyo kwa sababu havitatui mgogoro na tatizo lililojitokeza, bali ni uvunjivu wa haki za binadamu na vinapalilia zaidi hasama na kushawishi mwendelezo wa uvunjaji wa amani,” alisema.
Hadi sasa zaidi ya watu 23 wamejiorodhesha wakilalamikia ukiukwaji wa haki za binaadamu wa kupigwa na kuumziwa vibaya huku badhi yao wakiwa wamelazwa katika hospitali ya mnazi mmoja na vijana wawili wamepoteza maisha akiwemo Salim Hassan Mahaji na Hamad Ali Kaimu katika operesheni hiyo.
Kwa ujumla tokea kutokea kwa fujo zilizoanza wiki iliyopita na kusababisha kifo cha Koplo Said Abdulrahman jeshi la polisi limeanzisha msako mkali wa kuwasaka wahalifu na vikundi vyenye kuchochea vurugu huku vikifanya operesheni ya kushusha bendera za Uamsho na kuwapiga vibaya baadhi ya wananchi.

Mjomba wa marehemu huyo Salim Mussa Omar amesema kijana huyo alikufa akiwa ndani ya vyombo vya sheria amemuona wakati akiwa hapo hospitalini alikuwa na majeraha kichwani na michubuko sehemu mbali mbali za mwili wake.
Alisema kama askari walikuwa wengi wanaofikia 20 lakini ni sababu ipi iliyomfana asifikishwe mahakamani kwa kusomewa shitaka na waliamua kumpiga hadi kumuuwa.
NI lazima tufungua kesi latizo hawa wazee hawajuwi ni wapi pa kuanzia lakini mimi ni kama mwanawao nitachukua hatua za kisheria ili kulifikisha suala hili katika mahkama ili ijulikane ukweli”alisema.
Nae daktari dhamana wa hospitali kuu ya Mnazi moja Dakta Msafii Marijani ambae alimfanyia uchunguzi marehemu huyo amesema wamemfanyia uchunguzi wa ndani na nje lakini hajapata tatizo ambalo lingemsababishia kifo.
Tumempasua kichwani na kumfanyia uchunguzi na kuangalia kwa kina pamoja na kuwa ana michubuko mingi mwilini lakini si ambayo imesababisha kifo chake, kwa ufupi ripoti ya awali chanzo cha kifo hakijulikani maana hakuna jeraha kubwa lililosababisha kifo kwani mara nyingi chanzo cha kifo ni kutokwa na damu nyingi…lakini huwezi kuwaridhisha wana familia maana wana familia wanasema mambo mengi lakini wataalamu wa afya ndio wenye kujua” alisema Daktari huyo
Uchunguzi wa mwisho wa daktari ni kuwa amepata michubuko katika sehemu mbali mbali za mwili wake lakini haikusababishia michubuko hiyo kifo chake.
Baada ya kupokea tarifa kutoka kwa daktari aliyemfanyia uchunguzi jamaa wa marehemu Mohamed Ali Idi ambaye alishiriki katika ukaguzi wa maiti hiyo alisema anasikitishwa na ripoti iliyotolea ni ya kitalamu lakini si ya kibinadamu .
Huyu kijana wetu tumemkuta ametobolewa katika sehemu ya kichwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali ametobolewa sehemu ya bega ametobolewa sehemu ya ubavuni ana uvimbe ambao una rangi nyeusi ana uvimbe sehemu ya mgongoni mguuni unaonyesha amepigwa kipigo kilichosababisha uvimbe ule..
Majeraha hayo yanaweza kuwa sababu ya kifo chake polisi wametuulia halafu wanasema hakufa kwa kipigo majeraha aliyokuwa nayo yanatosha kuwa sababu ya kifo chake”alisema mwanafamilia huyo
Alisema Viongozi wanazungumza kuwa watachukuliwa hatua kwa yeyote atakaevunja amani kitendo walichokifanya polisi ni cha kusikitisha na serikali imesema yeyote atakaevunja sheria atachukuliwa hatua za kisheria.
Tunaiomba Serikali kuwachukulia hatua wale askari ambao wamefanya kitendo cha mauwaji wakamatawe kwani serikali imesema atakaevunja amani akamatwe basi na hawa waliouwa tunataka wachukuliwe hatua za kisheria .
Kitendo walichofanya askari ni kitendo cha uvunjifu wa haki za binadamu hivyo hatuna imani na jeshi la polisi
Mwenetu alimchukua akiwa mzima wala haumwi leo wamemua halafu wanatwambia hawajamua wao tuamini vipi wakati walimchukua akiwa mzima leo vipi wanaturejeshea maiti” alisema mwana familia huyo.
Hata hivyo ameiomba serikali ya mapinduzi kuwa makini na suala la uvunjifu wa haki za binadamu kwani jeshi la polisi
linahatarisha amani na kutaka hao waliouwa serikali iwadhibiti vyombo va ulinzi vimeshakuwa vinahataisha amani badala ya kuweka amani tunataka kuona seikali imechukua hatua juu tukio hili.

Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment