Moto wa
‘ajabu’ Pemba Nyumba zaendelea kuteketea L Wananchi wapiga kambi kusubiri
kuuzima
Na Masanja Mabula, Pemba
MOTO wa ajabu unaotokea katika mazingira ya
kutatanisha bado unaendelea kuteketeza nyumba na mali za wananchi wa kijiji cha
Tumbe Mashariki, jimbo la Tumbe, wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Moto huo ambao ulianza kuteketeza tokea Septemba 28
mwaka huu , tayari umeteketeza nyumba zipatazo 13 hadi sasa huku baadhi ya
nyumba nyingine zikishuhudiwa vitu vya ndani kama nguo zikiungua
huku makabati yakibakia salama.
na magodoro z ndivyo vinavyoteketea na nyumba
kubaki salama .
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya
wakaazi wa kijiji hicho walisema moto huo umekuwa ukitokea kutokana na imani za
kishirikina.
Walisema wananchi wa kijiji hicho wamepatwa na hofu
kubwa, kwa sababu moto huo hutokea katika mazingira yasiyotarajiwa.
Moto huo umesababisha hali ya umaskini kutokana na
wananchi kutumia muda wao mwingi ewakiwa nyumbani wakisubiri kukabiliana na
moto huo pindi unapotokea.
Wananchi hao walisema tokea kuanza
kutokea moto huo siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita shughuli za kiuchumi
zimezorota kwani wamekosa hata muda wa kushughulikia masuala ya uzalishaji mali
jambo ambalo limekuwa ni kikwazo katika kujiletea maendeleo.
"Matukio haya kwa kweli yansababisha hali ya
umaskini katika familia zetu kwani tunashindwa hata kwenda baharini kuvua, na
hata watoto wetu wanakosa muda wa kujisomea kutokana na wasiwasi uliotanda juu
ya usalama wa maisha kwa vile hatujui moto utatokea wakati gani,” alisema
Khamis Salim Kombo.
Aidha alisema cha kushangaza zaidi ni kuona wakati
mwengine kunaungua nguo na vitu vingine lakini mapaa ya nyumba yanabakia salama
licha ya moto huo kukiripuka hadi kwenye mapaa.
Alisema katika tukio lililotokea katika nyumba yake
bahasha ya nguo zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kwenda kuoshwa ziliwaka na
kuteketea pamoja na godoro huku kitanda kikibaki salama jambo ambalo
limewaweka katika wakati mgumu wa kujua chanzo cha moto huo .
Udadisi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa
kuzungumza na wazee alipofika katika katika kijiji hicho wakati
wa moto ukiendelea kuwaka , walisema kuwa zipo taarifa tofauti juu ya chanzo
cha moto huo ambazo zinahusishwa na masuala ya imani za kishirikina
kulikosababishwa na kusahauliwa kwa masuala ya kijadi.
Ikiwa katika eneo la tukio gazeti hili lilishuhudia
nyumba ya mzee Khatib Omar Kombo alikiwaka moto wakati mwenyewe akiwa amekwenda
msikitini na wala hakukuwa na dalili zozote za kuwepo moto ndani ya nyumba hata
hivyo wananchi waliwahi na kuuzima moto huo kabla ya kuleta madhara.
Taarifa zisokuwa rasmi zinasema
kuwa chanzo cha moto huo ni kukatwa mwembe kwa ajili ya kupisha
ujenzi wa soko kijijini hapo huku chanzo chengine cha habari kikieleza kuwa
baadhi ya wazee walipewa fedha kwa ajili ya kununua ng’ombe wa mji lakini
hawakutekeleza ahadi hizo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho Kamanda wa
Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Yahya Rashid Bugi
aliwataka wazee hao kuondoa imani za kishirikiana na kwamba njia pekee ya kuweza
kuondoa tatizo hilo ni kwa wananchi hao kuongeza idaba,maombi na dua.
"Acheni kuamini masuala ya kishirikiana
kuhusiana na matukio haya, nawaombeni kuwa njia pekee ni kuongeza ibada,
maombi, dua na sala na kwamba hii ni mitihani kutoka kwa Allah , endeleeni
kuwa wavumilivu," alishauri Kamanda Bugi.
Kufuatia kuwepo na matukio hayo wananchi wa Tumbe
Mashariki katika kijiji cha Kaliwa wameandaa maombi maalum kwa ajili kuomba
kuondoshewa kwa kadhia hiyo ambayo imenaweka roho za watu juu na kwapa wasi
wasi juu ya mustakabi wa maisha yao na mali zao.
Kijiji cha Tumbe kilikuwa maarufu sana kwa
masuala ya matambiko ya kijadi kila mwaka, kama ilivyo kijiji cha Makunduchi.
Chanzo: Zanzinews
No comments :
Post a Comment