Ya UAMSHO na Farid, CUF
na
Salum Msabaha
Written by Bablee // 20/10/2012
Kitendawili cha Ustaadh Farid kwamba alitekwa au alijificha, kinanikumbusha kile kitendawili cha CUF na Salum Msabaha.
Mara tunamuona Salum Msabaha amabe ni mjuzi wa dini ya kiislam (twaweza mwita ustaadh) kiongozi na mwanachama wa CUF kwenye ITV an TVZ akisema kwamba, yeye kwa hiyari yake, bila kushawishiwa wala kulazimishwa na mtu yoyote ameamuwa kuachana na CUF na kujiunga na CCM…..

Siku inayofuata kupitia ITV hiyo hiyo akiwa na Makamo mwenyekiti wa wakati huo Maalim Seif Sharif anaonekana tena akisema “Mimi Salum Msabaha bado ni kiongozi na mwanachama mtiifu wa CUF, CCM waliniteka na wakanipeleka kwenye TV wakanilazimisha niseme kwamba nimejiondoa CUF…” Baadhi ya Ma-CUF wakasema, alipokuwa akitangaza kujiondoa CUF alionekana akitetemeka, hivyo nikweli alikuwa anatangaza yale chini ya mtutu wa bunduki…sisi wengine bado hatujasahau.
Mara tunamuona na kushuhudia huyo ustaadh mcha mungu wetu huyu, anaejuwa kwamba kusema uwongo ni dhambi tunamuona akiwa ndani ya mwaganda ya CCM…naam tayari ni CCM kindaki ndaki, kada mkeretwa huku akipiga madongo CUF.

Ama hapa ndipo nnapoona ubaya wakuwaamini wale tunaowaona hawawezi kusema uwongo, eti ni ma ustaadh au ni wana siasa wakuheshimika. Jee kuna CUF anaweza kunambia msabaha alitekwa au alijitekesha?
Pamoja na historia hiyo bado sipingi uwezekano wa Sheikh Farid kuwa alitekwa…naam yeye si wa kwanza kutekwa na kupotea kabisa au kuachwa wakiwa hawana kucha, meno, macho n.k. Ila bado yatupasa kupima kwa uzito wake, tutoke nje ya “box”, tuwe na mawazo huru katika kukubali au kukataa uwepo wa utekwaji wa ustaadh Farid. Polisi kamwe hawatakubali kama walimteka, hata kama walifanya hivyo, na ustaadh Farid nae kamwe hatasema kama alijifcha, hata kama alijificha pale fuoni…Jee ukweli tutapata wapi?
Chanzo: Mzalendo
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment