Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 20, 2012

WANAVYOTUELEZA WATANGANYIKA!

                     KUHUSU UAMSHO NA SHEIKH
UST FARID
Mtanzania yeyote mwenye nia njema na Taifa lake ana haki ya kusikilizwa, haijalishi ana sababu ya msingi au hapana. Lakini haiwezekani ku-compromise na mtu yeyote mwenye nia ovu lakini anakuja kwa kusingizia kutetea haki za Wazanzibari.
Wazanzibari, kama walivyo Watanzania Bara, wanaweza kuwa na malalamiko yao, lakini hawawezi kuwakilishwa na watu walio wahuni ambao wanadai kuwa wanataka kuvunja mwungano lakini wanaenda kuchoma makanisa - Je, makanisa ndiyo yanayolazimisha mwungano? Wanaenda kuvunja maduka ya pombe na kuiba bia - Je bia ndiyo zinazolazimisha mwungano?


Wazanzibari kama hawataki mwungano, wajadiliane ndani ya nchi yao, ikiwezekana wapige kura ya maoni, na kisha waje kwenye serikali ya Mwungano na hoja waliyo nayo lakini siyo kuchoma nyumba za ibada - kwani hata mwungano ukivunjika ina maana Zanzibar watawanyima watu uhuru wa kuabudu? Kati ya watanzania walio wengi huko ulaya (kwa kuzingatia idadi ya wakazi katika nchi), wengi ni wa kutoka visiwani - Je, huko waliko, japo katika mataifa hayo idadi kubwa ni wakristo, waislam au wahindu wanazuiwa kujenga misikiti au kuabudu? Kama tunafurahia uhuru wa kuabudu tukiwa kwenye nchi za wenzetu, kwa nini kwetu hatupendi watu wote wafurahie uhuru wa namna hiyo hiyo?
Ndiyo maana ni muhimu sana, kwa sisi Watanzania wote, wakristo kwa waislam na wasio na dini, wazanzibari na Watanganyika kusimama kwa nguvu moja kuwakana na kuwapinga kwa nguvu zozote zile watu wanaotaka kututenga kwa misingi ya dini, iwe ni kwa kauli, kutenda au utoaji wa huduma. Hawa wanaoleta fujo hawana dini yoyote bali wanamtumikia ibilisi. Wanakuja na madai mchanganyiko, yasiyo na kichwa wala miguu lakini inaonekana dhamira yao kubwa ni kuleta vurugu. Wakifanikiwa kuwakorofisha Waislam na Wakristo, watakwenda kwa Washia na Wasuni, wakifanikiwa, watakwenda zaidi na kudai utawala wa sharia, n.k. n.k.
Huyu Fareed, inaonekana ni mfitini mkubwa. Dereva wake anasema, Fareed alishuka kwenye gari kwa hiari yake mwenyewe na kwenda kwenye gari nyingine aina ya Noah, yeye (dereva) aliambiwa akanunue umeme, aliporudi hakumwona Fareed wala ile gari. Leo Fareed anasema kuwa alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu, akamwambia wakutane msikitini, wakati akimsubiri huyo mtu, alimtuma dereva kununua umeme, wakati dereva alipoondoka huku nyuma gari ilikuja, alitoka mtu ndani ya gari akamfuata aliposimama na kumwambia kuwa yeye ni polisi, na kuwa amakuja kumchukua ili kumpeleka kituo cha polisi lakini hakupelekwa polisi.
Fareed anasema kuwa alitekwa na kufichwa sehemu asiyoijua kwa siku tatu, muda wote alifungwa kitambaa usoni na pingu mikononi kwa hiyo hakuwahi kuwaona watekaji, hakuona namba za gari, hakuona alipokuwa, na kwa muda wote hakula (hakupewa chakula wala maji) badala yake alipokuwa anaenda chooni alikuwa akinywa maji ya mfereji (Kipemba ina maana maji ya bomba). Maswali ya kujiuliza: Sura ya Fareed haielekei kabisa ni mtu aliyeishi kwa siku 3 bila kula, nini kilimfanya awe katika hali ya kawaida na siha njema kiasi kile? Kama hakuwa anaona na alikuwa amefungwa mikono wakati wote, aliwezaji kujua choo kilipo wakati hakuwa anaona? Aliwezaji kuona bomba la maji? Aliwezaji kufungua bomba la maji wakati alikuwa amefungwa? Ndiyo maana tunasema kuwa kupotea kwa Fareed kuna uwezekano mkubwa kulipangwa na kundi hili la Uamsho ili kutafuta kuungwa mkono na wafuasi wao wapate kuhalalisha uovu wao.
By Bart

Source: Wanabidii Forum


4 comments :

  1. Wewe muandishi wa makala haya uko hai au umekufa unataka mara ngapi wazanzibari waseme kama hawautaki muungano,wazanzibari hawautaki muungano kwa taarifa yako kama hujui,unazungumzia ulaya na uislamu kwani ulaya umekwenda peke yako? au ndio umehadhiwa ulaya kulivyo? wabaguzi number one ni ulaya katika mambo ya udini,soma tena ufaransa ,belgium,canada na kwingi kwengineko jinsi wanavyobanwa waislamu.
    Kwani vitimbi mnavyovifanya wakiristi kisirisiri waislamu hawavijui kuudhoufisha uislamu hasa hapa Tanzania mpumbavu weee,soma alama za wakati viongozi wa kikristo ndio wenye kutoboa siri hizo baada ya kusilimu na ndio sababu ya kusilimu kwa vile wameujua ukweli.
    Usiwe mjinga zanzibar itakuwa huru mkitaka msitake mbwa nyie,

    ReplyDelete
  2. Nafkiri wewe huna masikio, kwanza mfreji sio kipemba, ni kiswahili. Nyie mnajulia kiswahili mkianza darasa la kwanza, utajuaje kutofautisha kiswahili na kimakonde au kipemba.
    Ustadh Farid alisema kabisa kuwa hao watu walivaa mask usoni ndicho kisa cha kutowajuwa nani, Kawaida ya wafungwa hufunguliwa pingu akiwa katika chumba ambacho hawezi kukimbia, kwa maana hiyo, chooni hakukuwa na njia ya kukimbia na ndio maana ya kuenza kunywa hayo maji mferejini. Na pia hakukuwa na maana ya kufunikwa uso, kwani nyumba usiyowahi kuidhuru hata ukiiona chooni hutoweza kujuwa upo nyumba gani wala mtaa gani, na hilo ndio lengo la hao polisi walimkamata. Lengo lao sio kumfunika uso, bali ni kumueka gizani ili asijuwe ni nyumba gani aliyopelekwa. Upo ulaya gani wewe? au upo India?
    Kuhusu kula, mtu kawaida unao uwezo wa kukaa kwa muda wa masiku bila ya kula, na ukanywa maji tu na hata watu wasikujuwe na ukaonekana upo healthy, kwani nyinyi wakiristo si mnafunga kwa kunywa maji tu, kwa muda wa masiku, kama wewe hufanyi kawaulize walokelo.

    ReplyDelete
  3. Jaribuni kutumia lugha Nzuri zakukataa Makala yake au kukubaliana na makala yake. Na Muache kutumia Jazba na matusi... Hata hivyo kwa maoni yangu huyu kijana alieandika Hii makala au Blog ... Ni Mtanganyika ambae hata Kiswahili hakijui.

    Mfano Muungano anasema MwUngano...hichi siokiswahili safi kabisa ni kiswahili cha Kimasai..... Au Kimeru.....

    Jengine nimeona kwamba Blog haiwakilishi Zanzibar isipokua Mbuga za Tanganyika na Tanganyika kwa Ujumla na Sio Tanzania kama Alivyosema Muandishi. Picha Zote za Blog ni pichaza Mapori na The Tanganyika National Park . Amejaribu Kuiba na picha kutoka kwenye Lake Naikuru au Naivasha kule Kenya....

    Kumalizia Ndugu Muandishi unajua kwamba CCM na Makanisa Ndio Wanaoendesha Nchi ya Tanganyika kwakutumia Koti la Muungano. Na Mfumo wenu KRISTO wa Serikali ya Tanganyika-Muungano jacket... Ndio uliofanya Njama za Kuchoma Makanisa kule zanzibar.

    Wazanzibari ni Religions Tolerance- Makanisa na Wakristo kwetu (Wazanzibari) sio watu wa Ajabu- Bali ni Nduguzetu, tumeowana nao, tunasoma nao nimajirani zetu na tunaingiliana kwa Mila na Desturi.

    Ni nyinyi Watanganyika hasa wa Mikoani ndio muna Kasumba juu ya Dini kwasababu maisha yenu yote hamujui kutafautisha nini maana ya Dini na Imani... Ubinafsi, Uongo, Ulahai, wizi na kutokua Wakweli ndio Sera zenu. Na Ndiomaana Mukaufikisha Muungano hapa ulipofika kwa Tamaa zenu zakutaka kujifanya Watawala Weusi.

    ReplyDelete
  4. HUYU JAMAA ANAONEKANA NI MWENYE KUTAKA KUZIDI KUPALILIA FITNA MIONGONI MWA WAANZIBARI KWALENGO LA KUDHIBITI MFUMO ULIOPO SASA.WAZANZIBARI WAMEPOTEZA ROHO,MALI NA UTU WAO TOKA ZIANZE SIASA ZA VYAMA VINGI,NA HAYA YANAENDELEA.INAFAHAMIKA WAZI KWAMBA LENGO NI KUVIMEZA VISIWA NA NDIO MAANA TUNASHUHUDIA HIZI VURUGU AMBAZO ZINAANDALIWA NA WASIOIPENDELEA ZANZIBAR KUSIMAMA KUWA DOLA KAMA DOLA ZINGINEZO.INASIKITISHA KUONA WAZANZIBARI WANATUNGWA RISASI KAMA POPO NA MPAKA HII LEO HAKUNA ANAEZUNGUMZIA MAUAJI YA 2001.RAI NZURI NA YA KISTAARABUNA YA KIDEMOKRASIA NI KUITISHA KURA YA MAONI ILI MATAKWA YA WANANCHI YATEKELEZWE BILA YA UHASAMA WA RISASI

    ReplyDelete