Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 15, 2012

SCOTLAND NA UINGEREZA KUACHANA!

Kura ya maoni kuhusu kujitenga Scotland na Uingereza
Kura ya maoni kuhusu kujitenga Scotland na Uingereza
Viongozi wa serikali za Scotland na Uingereza wamekubaliana kuhusu kuitisha kura ya maoni ya kuamua suala la kujitenga Scotland na Uingereza. Michael Moore, Waziri wa Uingereza anayehusiana na masuala ya Scotland na Bi. Nicola Sturgeon, Naibu Waziri Kiongozi wa serikali ya Scotland wamefanya mazungumzo ya kujadili suala hilo. Wakati huo huo David Cameron Waziri Mkuu wa Uingereza na Alex Salmond Waziri Kiongozi wa Scotland wanatarajiwa kukutana leo Jumatatu kwa ajili ya kutia saini mwafaka wa kuitishwa kura ya maoni ya kujitenga Scotland na Uingereza.
Lengo la mkutano huo wa leo limetajwa pia kuwa ni kumaliza masuala ya mwisho yaliyobakia kuhusiana na mwafaka huo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, itabidi kura ya maoni ya kuamua kujitenga Scotland na Uingereza ifanyike kwenye msimu wa machipuo wa mwaka 2014. Matini kamili ya mwafaka huo watakabidhiwa Waziri Mkuu wa Uingereza na Waziri Kiongozi wa Scotland kwa ajili ya kujadiliwa na kupasishwa. Miongoni mwa masuala ya mwisho ambayo pande mbili zimekubaliana ni namna ya kudhamini fedha za kuitisha kura hiyo ya maoni. Itakumbukwa kuwa tangu mwaka 1707 wakati ilipoasisiwa nchi inayoitwa Briteni yaani "Great Britain" Scotland ilikuwa na serikali ya ndani ya kujiendeshea baadhi ya mambo yake kama vile Wizara ya Elimu, Afya na kujitungia sheria zake za ndani. Mwaka 1999 kuliasisiwa Bunge la Scotland na kuzidi kuifanya kuwa nchi huru, lakini pamoja na hayo bado ilikuwa chini utawala wa kifalme wa Malkia wa Uingereza. Kwa kweli kuvunja muungano na kujitenga na Uingereza ni ndoto ya miaka mingi ya wananchi wa Scotland na baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa kitakachofanyika kwenye kura ya maoni ya mwaka 2014 ni kupiga muhuri wa mwisho tu wa kujitenga Scotland na Uingereza. Wachambuzi hao wa mambo wanaamini kuwa, ni jambo linalowezekana kabisa kwa Scotland kujitenga na Uingereza. Waskochi wenyewe wanaamini kuwa kujitenga Scotland kutawafanya wawe na mwakilishi wao katika Bunge la Ulaya. Vile vile wanaamini kuwa tabia na tamaduni za Uingereza na Scotland hazifanani. Scotland ni nchi inayofuata mfumo wa Social Democrat wakati mfumo wa Uingereza ni wa kihafidhina. Weledi wa mambo wanaamni kuwa tofauti hizo kubwa zinalifanya suala la kuendelea kuungana nchi hizo mbili liwe gumu sana. Katika upande mwingine, chama cha taifa cha Scotland kinaamini kuwa ni haki ya kimsingi ya Waskochi kupewa fursa ya kupiga kura ya maoni ya kuamua mustakbali wa nchi yao. Kinaamini kuwa, hilo ni jambo ambalo kwa muda mrefu lilikuwa linapiganiwa na wananchi wa Scotland. Hata hivyo wako watu wanaopinga kuitishwa kura hiyo ya maoni. Jambo hilo linawafanya baadhi ya wafuatiliaji wa siasa za Uingereza waamini kuwa, kujitenga Scotland na Uingereza si jambo jepesi kama inavyofikiriwa. Hivyo kilichobakia ni kusubiri kuona kutatokea nini katika siku za usoni na katika kura hiyo ya maoni ya mwaka 2014.

Chanzo: http://kiswahili.irib.ir/uchambuzi/item/27093-kura-ya-maoni-kuhusu-kujitenga-scotland-na-uingereza

No comments :

Post a Comment