Spika Makinda ashiriki Mkutano wa 127 wa IPU, Mjini Quebec, Canada. Akutana na Spika wa Morocco
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mratibu wa
mahusiano baina ya Global Fund na Mabunge Duniani
Ndg. Svend Robinson, walipokutana kabla ya kuanza kwa mkutano
wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika
Mjini Quebec, Canada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimtambulisha Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Dr. Perpetua
Nderakindo Kessy kwa Balozi wa Tanzania Chini Canada
Mhe. Alex Massinda kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127
wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika
Mjini Quebec, Canada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifuatilia taarifa mbalimbali
na maazimio ya Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU)
wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 127 wa IPU Mjin Quebec, Canada.
Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada
Mhe. Alex Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
Mkurugenzi wa Maktaba na Utafiti wa Bunge Ndg. Kileo Nyambele
anaye muwakilisha katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashilila akishiliki
kikao cha makatibu wa Mabunge yote wanachama wa Mabunge ya
Dunia (IPU) katika Mkutano wa 127 wa chama hicho mjini Quebec,
Canada. Kulia kwake ni Afisa dawati la IPU kutoka Tanzania
Ndg. James Warbarg.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza ujumbe wa
Tanzania kupiga kura kuingiza agenda mojawapo kati ya
agenda 5 za dharura zilizowasilishwa kwa udharura katika
mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) ili
zijadiliwe pia. Tanzania iliungana na nchi za Afrika kupigia
kura agenda ya kujadili hali ya usalama katika nchi ya Mali
amoja na agenda iliyowasilishwa na Uingereza kujadili kwa
udharura swala la hatma ya Usalama na Misaada wa Kibinadamu
Nchini Syria na nchi Jirani. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania
Chini Canada Mhe. Alex C. Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
Spika wa Bunge akitoka katika ukumbi wa Mikutano mara baada
ya kumalizika kwa kikao cha kwanza katika Mkutano wa 127 wa
Chama cha Mabunge Duniani (IPU) mjini Quebec, Canada.
Kushoto kwake ni Mhe. David Kafulila anayehudhuria Mkutano huo pia.
Mhe. Anne Makinda akitoka katika Mkutano na Spika wa Bunge la
Morocco Mhe. Karim Ghellab kwa lengo la kufanya nae mazungumzo
ya faragha kuimarisha uhusiano baina ya mabunge ya Tanzania na Morroco.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisisitiza jambo wakati
alipokutana na Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab
kujadili namna bora ya kuimarisha mahusiano baina ya mabunge
ya nchi zao. Tanzania ilipeleka ujumbe wa Wabunge kutoka kamati
ya Mambo ya Nje, ulinzi na Usalama kutembelea Bunge la Morocco
Aprili mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina
ya nchi hizi mbili.
Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab akimkabidhi
Mhe. Spika zawadi mara baada ya kufanya nae Mazungumzo.
Ujumbe kutoka Bunge la Tanzania katika Mkutano wa 127 wa IPU
Mhe. Hamad Rashid na Mhe. Suzan Lyimo wakifuatilia kwa makini
mada kuhusu “Multilateralism and the role of parliament in
parliamentary diplomacy” wakati wa mkutano huo
Mjini Quebec, Canada.
Chanzo: Vijimambo
No comments :
Post a Comment