Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 21, 2012

UHAFIDHINA

UHAFIDHINA WATUMIKA UPYA KAMA MTAJI WA KUZUIA WIMBI LA MABADILIKO
Written by   //  21/10/2012
Alichokifanya Amani Karume katika kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ni pamoja na kulidhibiti kundi la wahafidhina lenye fikra za KISONGE ili wazanzibari waongozwe na uzanzibari wao katika kuyatafuta maslahi yao. Kuondoka kwa utawala wa Karume imekua ni sawa na kuirejesha Zanzibar katika mikono ya mtandao wa wahafidhina katika sura mpya kabisa na kuwateka nyara washirika wa Maridhiano na umoja huo wa kitaifa.
Viongozi wa CUF serikalini wamewachwa mayatima wa GNU wamebaki hawana sauti yoyote yenye nguvu, si kimaamuzi wala kiushauri. Akina Mansoor na Mzee Moyo ambao ni machampion wa maridhiano ndani ya CCM wanaendelea kutishwa kwa kauli kali kali, vitendo vya kuwakatisha tamaa, na kudharauliwa kutokana na misimamo yao ya kudai mabadiliko. Lengo ni wajue kwamba fikra za KISONGE zimerejea katika safu yake ya awali na zimeshika hatamu upya. Misingi ya fikra za maridhianao na serikali ya umoja wa kitaifa iliyotandikwa na Amani Karue na Maali Seif bila shaka ishapigwa teke.
Vitimbi kadhaa wa kadhaa vinavyoendelea dhidi ya UAMSHO, dhidi ya CUF, dhidi ya Mansoor, dhidi ya Mzee Moyo, dhidi ya Amani Karume nk ni suala moja tu vita dhidi ya umoja ambao wazanzibari wanaringia hivi sasa, hvyo vyote ni visu vinabadilishwa hiki na kile kuhakikisha kamba hii inakatwa ili tusambaratike tusifikie lengo tulilolikusudia. Wazanibari tusirudi nyuma wala tusitetereke tushikamaneni, wanaopigana kwa pamoja hushinda.
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA!

Waasisi wa serikali ya umoja wa kitaifa wakibadilishana mawazo
Source: Mzalendo

No comments :

Post a Comment