CHRONOLOGY YA MATESO YA WAZANZIBARI CHINI YA UTAWALA WA DR. SHENI KUANZIA SIKU
ALIOTEKWA SHEIKH FARID
Written by Ashakh (Kiongozi) // 25/10/2012
Najiuliza kama je tumo ndani ya Zanzibar au ukanda wa Gaza huko Palestina? Kwani haya maafa tunayoyashuhudia tunayofanyiwa sisi wazanzibari na vikosi vya dola ni sawa na yale wanayofanyiwa ndugu zetu wa Kipalestina huko ukanda wa Gaza. Jambo baya zaidi, yanafanyika ndani ya Mwezi huu mtukufu ambao Waislamu wa dunia nzima wako kwenye ibada ya Hijja huko Makka. Je Dr. Sheni utakwenda kujibu nini mbele ya Allah (S.W) juu ya ufisadi na dharau yako ya dini yake ndani ya mwezi huu mtukufu, na pia wewe kuamrisha na kusimamia Waislamu na Wasiowaislamu (Wazanzibari) kuuliwa, kunajisiwa, kupigwa, kufungwa, kuzuwiliwa kumuabudu Allah (S.W), watu na watoto kuteswa na kupigwa risasi, watu kujazwaa khofu, n.k. Je siku hiyo ikiwadia utamjibu Allah kuwa maafa haya hukuyajuwa?
Inshaallah naomba nikukukumbushe baadhi ya fisadi na hayo maafa unayoyasimamia na kuiendeleza ukiwa ndiwe mtawala ulioko madarakani.
Inshaallah naomba nikukukumbushe baadhi ya fisadi na hayo maafa unayoyasimamia na kuiendeleza ukiwa ndiwe mtawala ulioko madarakani.
Ukurasa huu naomba uwekwe kwenye mtandao huu wa mzalendo ili uwe kumbukumbu kwa vizazi vya baadae juu ya mateso yanayofanyika ndani ya Zanzibar chini ya utawala wa Dr. Ali Moh’d Sheni.
Yafuatayo ni baadhi tu ya maafa yanayoendelea kufanyiwa wazanzibari.
Tarehe 24-10-2012:
- Eneo la Kinuni mjini Unguja, vikosi vya dola viliwapiga wazanzibari kwa marungu, mateke, ngumi, fimbo, n.k. Baada ya mateso yote hayo, vikosi vya dola viliwatupa majeruhi hao kwenye gari kama mizigo. Kana kwamba mateso hayo hayatoshi, vikosi vya dola viliwamwaga majeruhi hao kwenye ukingo wa mlima wa Kinuni kama lori linavyomwaga kokoto, na hatiame wakaangukia bondeni wakiwa taabani.
- Vikosi vya dola, waliovalia kiraia, hapo uwanja wa Demokrasia (Kibanda Maiti) waliwapiga vibaya sana watoto wawili wa umri chini ya miaka 15 (kumi na tano) kwa kwa marungu, mateke, ngumi, fimbo, n.k mapaka wakawa taabani sana, huku wapitanjia wengi wakishuhudia mateso hayo. Baada ya mateso hayo watoto hao walikuwa taabani sana na wakawa wameinamia ardhi, na hapo ndipo vikosi vya dola vikaamua kuwafunga pingu na wakwa wanawapiga risasi za mpira miguuni. Na kisha majeruhi hao wakatupwa nay a gari aina ya Noah Baadhi ya walioshuhudia walikuwa wanatoka na machozi. Baadhi ya walioshuhudia waliwataja baadhi ya askari hao kwa majina ya Muhene na Haji Baunsa (ambaye pia ndie mmiliki wa gari hilo aina ya Noah).
- Huko Kidongochekundu, mjini Unguja, vikosi vya dola vinapita nyumba hadi nyumba na kuwapiga wazanzibari na kuwaumiza vibaya sana bila kosa lolote.
Tarehe 23-10-2012:
- Vikosi vya dola, vikiwa ndani ya gari nne (4) aina ya Landrover, waliwapiga vibaya sana watoto wanne wa umri chini ya miaka 13 (kumi na tatu) waliokuwa wanapita njia, kwa marungu, mateke, ngumi, fimbo, n.k mapaka wakawa taabani sana, huku wapitanjia wengi wakishuhudia mateso hayo lakini wakawa hawawezi kutoa msaada wowote. Baada ya mateso hayo watoto hao majeruhi waliokuwa taabani sana wakatupwa ndani ya magari ya Vikosi vya dola na haijuilikani walikopelekwa na walichoendakufanyiwa mbele ya safari.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment