Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 25, 2012

Viongozi wa UAMSHO warudishwa tena rumande

Thursday, October 25, 2012.

Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Abdallah Juma kushoto na Salim Tawfik wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu kujitoa kwao siku ya leo katika kesi hiyo kutokana na usmbufu wanaofanyiwa wateja wao wa kuhawangaishwa na kukosa kupelekwa Mahakama ya Kwerekwe kwa muda muafaka.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
VIONGOZI wanane wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) huku wakiwa wamenyolewa ndevu wameshitakiwa mahakamani kwa madai ya kuhatarisha amani Zanzibar…
Wakitarajiwa kufikishwa mahakamani jana kuendelea na kesi yao ya awali kwenye Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwereke, viongozi hao walipelekwa Mahakama Kuu Vuga mjini hapa na kufunguliwa mashitaka mapya.
Wakati wanafikishwa mahakamani kwa siku ya kwanza Jumatatu iliyopita washitakiwa wote walikuwa na ndevu videvuni mwao lakini jana walikuwa wamenyolewa. Na jambo hilo kuzua gumzo kubwa miongoni mwa jamii.
Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee Ibrahim ameeleza kwa mamlaka aliyopewa na sheria ya Usalama wa Taifa kifungu cha 10 anawafungulia mashitaka watu hao akiwemo Sheikh Farid Hadi Ahmed ambaye kutoweka kwake hivi karibuni kulizua ghasia kubwa Zanzibar.
Wengine waliofikishwa mahakamani ni masheikh Msellem Ali Msellem, Mussa Juma Issa, Azzan Khalid Hamdan, Suleiman Juma Suleiman, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar.
Walisomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Raya Msellem liyekuwa akisaidiwa na Rashidi Fadhili na Ramadhan Nasibu mbele ya Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar, George Kazi.
Hati ya mashitaka inasema kuwa kuanzia Oktoba 17 hadi Oktoba 18 mwaka huu katika barabara kadhaa za Mkoa wa Mjini Magharibi washitakiwa hao wanadaiwa kuwachochochea wafuasi wao kuharibu barabara, kuvunja majumba, kuharibu vyombo vya moto na kuleta hasara ya sh. 500 milioni.
Shitaka lingine wanadaiwa kuwa kati ya Mei 26 hadi Oktoba 19 mwaka huu katika mandamano yaliyofanyika Lumumba, Msumbiji, Fuoni Meli sita na Mbuyni Unguja waliwshawishi watu wengine ambao hawapo kortini kufanya ghasia na kuhatarisha amani.
Jumatatu iliyopita watu 7 bila kuwemo Ghalib Ahmada Omar walifikishwa katika Mahakama ya Mwanakwerekwe kwa madai ya kufanya uchochezi katika mhadhara walioufanya Agosti 17 mwaka huu.
Waliporudishwa tena Mahakama ya Mwanakwereke kwa kesi yao ya awali haikuweza kusikilizwa kwa vile halimu hakuwepo. Washitakiwa hao wamerudishwa rumande hadi Novemba 7 kesi yao ya Mwanakwerekwe itakposikilizwa na Novemba 8 siku ya kesi ya Mahakama Kuu.
Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani bila ya kuwa na mawakili baada ya mawakili wao, Salim Tawfik na Abdallah Juma kujitoa katika kesi hiyo kwa madai ya kuwa wateja wao wanadhalilishwa.
Wakizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu Vuga, mawakili hao walisema kitendo cha serikali kuwashikilia wateja wao na kushindwa kuwaleta mahakamani ni dalili tosha ya kuonesha haki haiwezi kutendeka kwani ni kitendo kinachokwenda kinyume na sheria za kimataifa na sheria za nchi hasa kwa kuzingatia kupewa dhamana ni haki ya kila raia.
“Inaonesha hapa haki haiwezi kutendeka dalili zimeanza kuonesha mapema kwa sababu kwanza wamezuiliwa kupewa dhamana wakati pande zote mbili hazikuwa na pingamizi ya kutoa dhamana lakini mahakama ndio inakataa kutoa dhamana, lakini jambo jengine na la kushangaza walitakiwa kuletwa hapa mahakamani lakini sisi tumekuja hapa mahakama ya Mwanakwerekwe tunasubiri wateja wetu hawajaletwa mpaka saa 5:30 asubuhi tunaulizia tunaambiwa twende Vuga na tunafika hapa Vuga hakuna mtu kwa hivyo tunajitoa katika hii kesi kwa leo (jana) ili kufikisha ujumbe wa serikali kwamba hawawatendei haki wateja wetu,” alisema Tawfik.

No comments :

Post a Comment