Written by Harith // 21/10/2012
SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUPITIA TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR IMESITISHA MATANGAZO YA VIPINDI NA TAARIFA ZOTE ZINAZOHUSIANA NA HARAKATI ZA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR.
KWA MUJIBU WA BARUA ILIYOSAMBAZWA KWA VITUO VYOTE VYA RADIO NA TELEVISHENI HATUA HIYO INA LENGO LAKUKABILIANA NA MACHAFUKO YA NDANI YA NCHI.
TAARIFA HIYO IMEBAINISHA KUWA KUMEJITOKEZA BAADHI YA VIKUNDI VYA WATU WANAOJIITA UAMSHO NAKUSABABISHA VURUGU NDANI YA NCHI.
TAARIFA HIYO IMEBAINISHA KUWA KUMEJITOKEZA BAADHI YA VIKUNDI VYA WATU WANAOJIITA UAMSHO NAKUSABABISHA VURUGU NDANI YA NCHI.
KULINGANA NA TAARIFA HIYO YA SEREKALI KITUO CHOCHOTE KITAKACHOKWENDA KINYUME KINYUME NA AGIZO HILO BILA YA IDHINI YA TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR HATUA ZINAZOFAA ZITACHUKULIWA.
WAKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA KHABARI HIZI BAADHI YA WANANCHI WAMELALAMIKIA KITENDO HICHO WALICHOSEMA KUWA KINA LENGO LAKUDHIBITI UHURU WA HABARI KWA KULINDA MASLAHI YA SEREKALI.
licha ya hatua hiyo ya serekali wananchi wamesema watatumia mtandao wa internet na simu zao za mkononi ili kupata taarifa mbali mbali kuhusu harakati za ukombozi wa zanzibar kutoka katika makucha ya tanganyika.
aidha wananchi hao wameeleza kuwa kitendo cha serekali kuzuia uhuru wa maoni ni chakidikteta na hakikubaliki katika mfumo uliopo wakidemokrasia na serekali ya umoja wakitaifa iliyopatikana kwa njia ya maridhiano yakisiasa kati ya ccm na cuf.
sambamba na hayo viongozi watano wa jumuiya na taasisi zakiislam zanzibar wamekamatwa na jeshi la polisi nakufunguliwa mashtaka yakuvuruga amani ya nchinakusababisha uharibifu wa mali za serekali,chama cha mapinduzi na za baadhi ya wanmsanchi.
viongozi hao ni amiri mkuu wa jumuiya na taasisi zakiislam zanzibar ambaye pia ni amiri mkuu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar fadhilatu sheikh msellem bin ali na msemaji wa harakati hiyo ambaye pia ni amiri mkuu wa jumuiya ya maimamu zanzibar sheikh farid hadi ahmed na naibu amiri wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar al-ustadh azzan khalid hamdan.
wengine ni al-ustadh mussa juma aliyewahi kukamatwa miezi kadhaa iliyopita na ustadh hassan bakari kutoka jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar.
kukamatwa kwa viongozi hao kumeelezwa na wananchi kuwa kunaweza kuvuruga tena hali ya amani ya nchi iliyopo yao.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment