22/10/2012
Kwa niaba ya Afisa Utawala wa wa Jumuia ya Wazanzibari walioko Canada, nachukuwa fursa hii kuwatangazia
Wazanzibari wote waishio katika maeneo ya GTA, Niagara, Hamilton, ST Catherine New Market na Oshwa, kuwa kutakuwa na mkusanyiko wa Eid al-Adh-ha siku ya Jumamosi tarehe 27 Oktoba kuanzia saa tisa jioni katika ukumbi wa Lawrence Heights Community Center iliyok karibu na kitu cha Subway ya Lawrence West. Kwa wale watakaochukuwa Subway wanaweza kushikia Lawrence West Station na wale wanao drive kutokea West wanaweza kwenda na Allen Rd na baadaye kuingilia Flemington Rd.
Sadaka za vyakula na vinywaji zinakaribishwa kwa atakayekuwa na nafasi.
Shukrani
No comments :
Post a Comment