Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 5, 2012

AZIMIO YA MAFUNZO YA SIKU MBILI YA MAKATIBU WENEZI


Written by   //  05/12/2012

CCM NEC NOV 3
MAAZIMIO YA MAFUNZO YA SIKU MBILI YA MAKATIBU WENEZI WA MIKOA, WILAYA NA MAJIMBO YOTE YA UNGUJA TAREHE 04/05/2012 KATIKA UKUMBI WA AFISI KUU YA CCM KISIWANDUI.
1)MAPINDUZI
Tunalaani mbinu na njama zote zinazofanywa kwa makusudi na wapotoshaji ya kupotosha ukweli dhidi ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na manufaa yake kwa waafrika yaliyotuletea uhuru wa kweli wa kujiamulia mambo yetu na kutaka kuturejeshea utumwa, ubwana na utwana.
(2)HISTORIA
Somo la historia kuendelea kufundishwa ili vijana wajue ukweli wa historia ya ukombozi wan chi ya yao ambayo Wazee wetu walipitia katika kutafuta Uhuru wa Mzanzibari.
(3)AHADI
Makatibu Wenezi tunaahidi kuwa kuanzia hitimisho la Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma wa 14/11/2012 na kupata safu mpya ya uongkozi, sasa kila Katibu Mwenezi kwa nafasi yake alipo atatekeleza , kuhamasisha Siasa na Itikadi sahihi ya CCM kwa maana ya CCM KWANZA mtu baadae.
(4)PONGEZI
Tunapongeza kwa kuchaguliwa ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndugu Ali Mohammed Shein kuwa Makamo Mwenyekiti kwa upande wa Zanzibar na Ndugu Philip Jafet Mangula kuwa Makamo Mwenyekiti kwa upande wa Tanzania Bara kwa ushindi wa kishindo.
Pia tunaunga mkono hotuba za Mwenyekiti wa CCM taifa ndugu Jakaya Mrisho Kikwete alizotoa katika Mkutano Mkuu mjini Dodoma na pia tunaunga mkono hotuba ya Makamo Mwenye kiti wa CCM Zanzibar Ndugu Ali Mohammed Shein aliyoitoa katika viwanja vya Demokrasia Kibandamaiti tarehe 17/11/2012 na kukiomba chama kusimamia ipasavyo utekelezaji wa hotuba hizo.
(5)HATUA DHIDI YA VIONGOZI WAPOTOFU.
Tuntamka na kutaka viongozi waliojidhihirisha wazi kukataa na kupinga masharti ya uanachama katika ibara ya 3(a-f) ya ilani ya itikadi ya CCM ya Muundo wa Serikali mbili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wafukuzwe uwanachama mara moja.
(6)TAMKO
Baadhi ya wazee waasisi wa TANU na ASP kuacha kupotosha ukweli wa historia ya nchi na chama kwa ujumla ili kuwezesha vijana kufaidika na matunda ya Muungano wa Tanzania na Matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar kama walivyofaidi katika enzi zao.
(7)MIKAKATI
Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wanaotokana na CCM kuwashirikisha ipasavyo makatibu wa itikadi , siasa na uenezi wa ngazi husika katika kutekeleza shughuli na MIkutano mbalimbali ya kimaendeleo ili kuwawezesha kufahamu zaidi utekelezaji wa majukumu yao kwa manufaa ya CCM.
(8)SISITIZO
Tunasisitiza na kuhimiza kuwa azimio la mkutano mkuu wa CCM Dodoma wa kuiwezesha na kuiimarisha idara ya itikadi , siasa na uenezi ngazi ya Mikoa, Wilaya na Majimbo kwa kupatiwa Nyenzo na Taaluma zaidi katika kufanikisha Majukumu yao ipasavyo
(9)KUTEKELEZA AHADI
Serikali kupitia Watendaji wake wanaotokana na CCM kuharakisha kutekeleza ahadi zake kwa Wananchi hususan kuharakisha kumaliza tatizo la mgao wa umeme, Maji safi na salama, Huduma za afya na Elimu pamoja na kuimarisha sekta ya Kilimoili kuwawezesha wenezi kutangaza mafanikio hayo kwa Umma na kuwa kivutio cha kupata wanachama wapya.
(10)TAARIFA
Kwa kuwa rais wa Zanzibar ni rais Mtendaji ni muhimu kushuka kwa wananchi kujua kwa undani taarifa anazopewa na watendaji wake ili kuwezesha kuwa na taarifa sahihi za utekelezaji wa ilan ya CCM.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment