Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 23, 2012

BLW - ZANZIBAR: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Written by   //  22/12/2012

Ndugu Waandishi wa Habari.
Baraza la Wawakilishi limechukua hatua mbali mbali katika kuhakikisha kunakuwa na ushiriki mkubwa zaidi wa wananchi hasa katika mchakato wa utungaji wa Sheria za nchi. Miongoni mwa hatua hizo ni kusomwa kwa miswada kwa mara ya kwanza katika mkutano mmoja na kujadiliwa na kupitishwa katika Mkutano wa Baraza unaofuatia ili kutoa fursa ya kutosha kwa wananchi kushiriki katika kutoa maoni yao.
Kufuatia mabadiliko ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuelekeza miswada ya Sheria kusomwa kwa mara tatu, Kanuni inaelekeza baada ya miswada hiyo kusomwa mara ya kwanza itangazwe kwa wananchi ili waifahamu miswada hiyo na waweze kushiriki kutoa maoni yao mbali mbali.
Ni matarajio yetu kuwa maoni yatakayotolewa na wananchi mbali mbali, kwa kiasi kikubwa yatazisaidia Kamati zitakazoichambua miswada hiyo ili kuifanya miswada hiyo kuwa bora zaidi na hatimaye kupata sheria zitakazozingatia kwa upana zaidi maslahi ya wananchi.
Katika Mkutano wa Kumi wa Baraza la Nane la Wawakilishi miswada ifuatayo itajadiliwa.
1. Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Usafiri wa Baharini Nam. 5 ya mwaka 2006
2. Msawada wa Sheria ya Kuanzisha Shirika la Utangazaji Zanzibar, kazi, majukumu na utawala wake pamoja na mabo mengine yanayohusiana na hayo
3. Mswada wa Sheria ya kuanzisha Shirika la Meli Zanzibar, kazi, uwezo na mambo mengine yanayohusiana na hayo
4. Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ruzuku kwa Vyama vya Siasa Nam. 6 ya mwaka 1997 na mambo mengine yanayohusiana na hayo
Ili kupata michango mbali mbali wananchi wanakaribishwa kutoa maoni kuhusia na miswada
hiyo. Maoni yawasilishwe kwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi kwa njia ya maandishi, si zaidi ya tarehe
4 Januari, 2013.

Aidha, nakala za miswada hiyo zinapatikana katika Afisi ya Katibu wa Baraza la Wawakilishi na
hivyo kila mwananchi atakayependa, anaweza kuomba kupatiwa nakala hizo.
Maoni yatumwe kupitia anauni zifuatazo:-
1. Sanduku la Posta (S.L.P. 902, Zanzibar)
2. Barua pepe (zahore@zanlink.co au
3. Yaletwe Afisi ya Baraza iliyopo Chukwani
Imetolewa na:
…………………………………
Amour M. Amour
Kny: KATIBU,
BARAZA LA WAWAKILISHI,
ZANZIBAR.
Tarehe 21 Disemba, 2012
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment