Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 2, 2012

ISMAIL JUSSA ASEMA: SHAME ON YOU SMZ!!!

Beit el Ajab Laporomoka (House of Wonders) Shame on You
Written by   //  01/12/2012  

Jussa akipigania kwenye BLW kukarabatiwa kwa Beit-el-Ajaib na 
majengo ya Kasri, 
lakini kelele zake ziliangukia kwenye masikio ziwi na pofu ya SMZ!

beit el ajaib

Aibu iliyoje leo kufikia Beit-el-Ajaib kuanguka baada ya Serikali kupuuza hatua zote za kuwazindua kuwa jengo hilo liko katika hali mbaya. Katika kikao cha Bajeti cha Baraza la Wawakilishi cha mwezi Juni/Julai 2011 na 2012 nilizungumzia suala la uwezekano wa majengo haya ya kihistoria kuanguka kutokana na kutotunzwa au kufanyiwa matengenezo. Nikaandika na swali maalum kuhoji matengenezo ya majengo hayo hasa baada ya mradi wa MACEMP unaofadhiliwa na nchi wahisani na mashirika ya kimataifa kuwa na fungu la matengenezo la majengo ya Kasri (Palace) na Beit-el-Ajaib. Kama kawaida ya majibu ya Serikali, tuliambiwa, ‘Tusiwe na wasiwasi’. Nikatahadharisha kuwa binafsi nimeyatembelea majengo hayo mawili kuona pamefanyika matengenezo gani kutokana na fedha zilizotengwa, na kuona hapana matengenezo ya maana. Nikajibiwa, ‘Tutafuatilia’. Sasa leo hii turathi ya kitaifa (national heritage) ambayo ni jengo la kwanza refu katika Afrika Mashariki, la kwanza kuwa na umeme na la kwanza kuwa na lifti kiasi cha kuitwa Jumba la Ajabu (House of Wonders) limeanguka kwa uzembe wa Serikali. Shame on them!
Ismail J Ladhu

No comments :

Post a Comment