Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 6, 2012

Jamuhuri ya Watu wa China yasisitiza kuwa na ushirikiano mkubwa na Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza 
na Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya watu wa China Bibi Chen Qiiman 
hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea 
zawadi ya picha za kuchora kutoka kwa Balozi wa Jamuhuri ya 
Watu wa China Bibi Chen Qiiman.

Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar 
Bibi Chen Qiiman pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
Balozi Seif Ali Iddi wakifurahia moja ya picha za michoro ya 
opera iliyosanifiwa na wataalamu wa fani ya sanaa kutoka China.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi 
akipokea moja ya Seti ya TV kati ya mbili alizopatiwa zawadi kutoka 
Ubalozi Mdogo wa Jamuhuri ya Waztu wa China hapa 
Zanzibar kwa ajili ya Ofisi yake.
Na salma Salma - ZNZ
Jamuhuri ya Watu wa China imesisitiza kwamba Zanzibar itaendelea 
kuwa mshirika wake Mkuu katika kudumisha udugu na ushirikiano wa 
muda mrefu uliojengeka kupitia Nyanja za maendeleo, Kiuchumi na 
ustawi wa Jami.i
Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Bibi 
Chen Qiiman ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa 
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika hafla fupi ya kumkabidhi 
zawadi ya Seti mbili za Tv kwa ajili ya Ofisi yake.

Balozi Chen Qiiman alisema ushirikiano wa sekta ya afya hivi sasa 
umepiga hatua kubwa ambapo vipindi maalum vimeandaliwa kwa 
pamoja kati ya wataalamu wa afya wa pande hizo mbili katika 
kuwafundisha wananchi kuelewa vyema elimu ya afya.

Alisema Taaluma hiyo imeelekezwa zaidi kwa wananachi wa kawaida 
hasa wale wa vijijini kuweza kujipatia elimu ya kujikinga na maradhi 
mbali mbali kupitia vipindi hivyo muhimu.

Akizungumzia sekta ya Ujenzi Balozi Chen Qiiman aliipongeza Serikali 
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua zake za ushirikiano inayotowa 
kwa wahandisi wa Kampuni za Jamuhuri ya Watu wa China 
zinazoendeleza ujenzi wa majengo tofauti hapa Zanzibar.

Balozi Chen alisema hatua hiyo ya ushirikiano imetowa fursa kwa 
wajenzi hao kuendeleza harakati zao za ujenzi na kufikia muda 
muwafaka wa kukamilisha kazi zao kwa mujibu wa mikataba 
inavyofungwa.

Hata hivyo Balozi Chen alisema zipo hitilafu za kiufundi zilizojitokeza 
wakati wa ujenzi wa jengo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa 
Zanzibar ambazo tayari zimeshapatiwa ufumbuzi na vifaa kwa ajili 
ya marekebisho ya hitilafu hizo vitawasili nchi muda wowote kuanzia 
sasa ili kukamilisha ujenzi huo.

Akitoa shukrani zake mara baada ya kupokea zawadi hizo za Seti za 
Tv Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema 
China na Zanzibar zina Historia ndefu ya ushirikiano ambao unafaa kudumishwa kwa maslahi ya wananchi wa Nchi hizo mbili.

Balozi Seif alisema mpango maalum wa Jamuhuri ya Watu wa China 
wa kuwapatia mafunzo watendaji wa Serikali, Viongozi pamoja na 
misaada ni uthibitisho kamili wa kukuwa kwa ushirikiano huo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuhakikishai Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo hapa Zanzibar Bibi Chen Qiiman 
kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano 
wa karibu kwa ndugu zao wa China wanaotoa huduma hapa Zanzibar 
katika Nyanja tofauti.

Alimuomba Balozi Mdogo wa China kufikiria kuongeza fursa zaidi za 
masomo ya ngazi ya juu kwa wanafunzi wa Zanzibar katika ngazi ya 
udaktari ili kupunguza uhaba wa madaktari uliopo nchini.


Chanzo: Vijimambo

No comments :

Post a Comment