ZIPO sababu nyingi zinazoelezwa kushawishi Tanganyika na Zanzibar kuunda Muungano ikiwa ni pamoja na kufanana kwa historia pamoja na mahusiano ya karibu wakati wa ukombozi wan chi za Afrika kutoka mikononi mwa wakoloni.
Ni miaka 48 sasa tangu Muungano huo ufanyike na kutengeneza historia kwa kuwa ni miongoni mwa mataifa yaliyodumu katika muungano.
Muungano huu umekuwa na mjadala mkubwa katika kipindi cha hivi karibuni ambapo kila upande umekuwa na manung’uniko ya kutonufaika na Muungano huu.
Moja kati ya mambo yanayoleta suitafahamu ni suala la gesi na mafuta ambalo limeonekana kuzua mjadala mkubwa wenye mgongano wa kimaslahi na hata kuonekana kuwa yapo makosa yaliyofanyika awali wakati wa kujadili jambo hilo.
Ukiangalia takwimu za hivi karibuni zinaonyesha Pwani ya Afrika Mashariki kuna jumla ya futi za ujazo trilioni 33 za gesi asilia zilizogunduliwa ambapo futi za ujazo trilioni 20 kati ya hizo zimeshapimwa na kuonekana na thamani ya dola 6 trillioni.
Ukiangalia takwimu za hivi karibuni zinaonyesha Pwani ya Afrika Mashariki kuna jumla ya futi za ujazo trilioni 33 za gesi asilia zilizogunduliwa ambapo futi za ujazo trilioni 20 kati ya hizo zimeshapimwa na kuonekana na thamani ya dola 6 trillioni.
Kutokana na utajiri huo, wataalamu nao wanasema endapo kasi ya utafutaji mafuta itaendelea katika kipindi cha miaka 2 ijayo basi Tanzania itaweza kuwa kati ya nchi mbili za Afrika zenye utajiri mwingi zaidi wa gesi asilia ikifuatia Nigeria inayoongoza kwa futi za ujazo trilioni 189.
Upatikanaji wa gesi asilia na mafuta ndiwo unaodhaniwa kuwa matokeo ya mgogoro unaoonekana kwa sasa baina ya Wazanzibari na Watanganyika kiasi cha kuonekana kuwa pengine nyongeza ya jambo hilo katika mambo ya Muungano haikufuata taratibu za kisheria.
Hali hiyo inamsukuma Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutoa mapendekezo kuhusu utatuzi wa mgogoro huo akisema kipindi hiki ni mwafaka kwa suala hilo kutolewa uamuzi kupitia Katiba Mpya.
Zitto anasema kumbukumbu ya Muungano inaonyesha kuwa baada ya kuundwa Muungano na Hati ya Muungano kusainiwa, suala hilo halikuwamo katika orodha ya mambo 11 ya Muungano.
Anasema makosa yalifanyika mwaka mmoja baada ya Muungano ambapo waliunda Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC) kwa amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano mwaka ya 1960.
Anasema makosa yalifanyika mwaka mmoja baada ya Muungano ambapo waliunda Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC) kwa amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano mwaka ya 1960.
Kutokana na amri hiyo ya Rais, Zitto anasema TPDC haikupewa mamlaka ya kimuungano ambapo mipaka yake iliainishwa kuwa ni Tanzania Bara peke yake.
Zitto anasema uaamuzi huo haukufahamika kama ilikuwa ni bahati mbaya au makusudi au kupitiwa kwa viongozi wakati huo na kwamba ni makosa ambayo yalipaswa kurekebishwa mapema.
“Kwasababu Shirika la TPDC limekuwa likifanya kazi ya kusimamia sekta ya mafuta na gesi ikiwamo kutoa vibali vya kutafuta mafuta, kuingia mikataba na makampuni ya kimataifa na kuisimamia mikataba hiyo,” anasema na kuongeza,
“Miongoni mwa mikataba iliyosainiwa na shirika hilo, baadhi yake ilikuwa katika maeneo ambayo kama leo hii kusingekuwa na Muungano, basi yangeendelea kutambuliwa kuwa ni maeneo ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Zitto anasema mikataba yote ya utafutaji na uchimbaji mafuta inaingiwa na Waziri wa Nishati na Madini ambaye hahusiki na Muungano na kwamba hakuna taratibu zilizowekwa kimaandishi kwamba eneo lililokuwa mali ya Zanzibar, kusainiwa na mawaziri wa pande zote mbili.
Anatoa mfano kwa kusema; “Mwaka 2000 Shirika hilo na Wizara ya Nishati waliingia mkataba na makampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi katika vitalu kadhaa sanjari na kitalu kilichopo kati ya Pemba na Tanga ambacho kina dalili za kuwapo mafuta kutokana na ‘Oil sips’ inayoonekana mara kwa mara.
“Vitalu hivi vipo katika eneo la iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kabla ya Muungano, lakini Serikali ya Zanzibar ilikataa shughuli zozote kufanyika mpaka suala hilo lipatiwe ufumbuzi,” anasema Zitto.
Uamuzi huo wa Serikali ya Zanzibar ni uamuzi ambao ulileta mjadala mpana sana katika masuala ya Muungano na hata kupelekwa katika vikao vya masuala ya Muungano.
Zitto anasema uamuzi wa Bunge la Muungano kuliweka suala hilo kwenye mambo ya Muungano ni makosa yaliyofanyika na kwamba njia sahihi ya kuamua mgogoro uliopo ni wakati huo ambapo kuna mchakato wa mabadiliko katika Katiba.
Zitto anasema uamuzi wa Bunge la Muungano kuliweka suala hilo kwenye mambo ya Muungano ni makosa yaliyofanyika na kwamba njia sahihi ya kuamua mgogoro uliopo ni wakati huo ambapo kuna mchakato wa mabadiliko katika Katiba.
“Ni dhahiri kwamba kama ni kusahau basi kulikuwa na usahaulifu mkubwa ambao hauwezi kuvumiliwa na mtu yeyote, Katiba Mpya ndio inaweza kuwa suluhisho,” anasema Zitto.
Zitto anasema kipindi cha miaka kumi kimepita bila mafanikio ya kufanyia ufumbuzi hivyo mjadala wa Katiba Mpya unaoendelea uliangalie suala hilo na ikiwezekana kila upande wa Muungano ujitegemee kuchimba na kukusanya mapato yake ya mafuta na gesi asilia.
“Si hivyo jambo lingine ni kuhakikisha Shughuli za utafutaji wa mafuta katika vitalu vyenye mgogoro baina ya pande hizo mbili zinaendelea na Zanzibar inatakiwa kuanzisha shirika lake la mafuta na itofautishe shughuli za utafutaji na biashara,” anasema Zitto.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji, aunga mkono hoja hiyo na kusema kuwa suala hilo liliingizwa katika orodha hiyo kwa kupigiwa kura na Bunge la Muungano na kuungwa mkono kwa theluthi mbili ya Wabunge wa pande zote za Muungano.
Profesa Shivji amesema kuwa taratibu zote za kisheria chini ya Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hayati Aman Abeid Karume zilifuatwa.
Aidha Profesa Shivji anasema kuwa suala hilo linahitaji hekima na busara katika kulitafutia ufumbuzi wake ili kuepuka matatizo yaliyojikeza katika mataifa ya Angola, Nigeria na Ghana ambapo chanzo chake kinaelezwa kuwa ni mafuta.
Chanzo: zalendo
No comments :
Post a Comment