Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 23, 2012

Meli za mitumba kunyimwa usajili Zanzibar

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Rashid Seif Suleimani


NA MWINYI SADALLAH

23rd December 2012


Meli  yenye umri wa miaka 15 tangu zianze kutoa huduma haitosajiliwa au kupewa lesseni ya kuchukua abiria na mizigo visiwani Zanzibar.

Mapendekezo hayo yamo katika marekebisho ya muswada wa sheria ya usafiri wa baharini namba 5 wa mwaka 2006 unaotarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Januari, mwakani.

Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Rashid Seif Suleimani, ambapo meli zenye umri huo itakuwa marufuku kusajiliwa na kutoa huduma katika mwambao wa Tanzania.

“Hakuna meli ambayo itazidi umri wa miaka 15 tokea tarehe ya kutumika kwake, itakayosajiliwa au kupewa leseni kwa ajili ya kuchukua abiria na mizigo Zanzibar,” kifungu cha 17A(1) kimesema cha muswada huo.

Aidha muswada huo umeleeza kwamba chombo chochote kinachotua nchi kavu, ikiwa asili ya utengenezaji wake si kwa ajili ya kuchukua abiria, hakitosajiliwa au kupewa lesseni kwa madhumuni ya kuchukua abiria ndani ya Zanzibar.

“Hakuna meli itakayosajiliwa au kupewa leseni kwa madhumuni ya kuchukua abiria ndani ya Zanzibar ikiwa meli hiyo imebadilishwa kutoka katika asili ya utengenezaji wake,” sehemu ya muswada huo umesema.

Muswada huo umefafanua kuwa mabadiliko hayo yanahusisha ikiwemo kubadili muundo wa meli, mashine za umeme, vyombo vya mawasiliano, winji au vitu vinavyofanana navyo.

Aidha kifungu cha 27 (3) cha muswada huo kimepiga marufuku mtu yeyote au wakala kumuajiri baharia katika meli za Tanzania Zanzibar au za kigeni bila kupata lesseni iliyo katika mfumo ulioelezwa na na mamlaka ya usafiri wa baharini Zanzibar.

Muswada huo umeeleza kwamba madhumuni ya marekebisho ya muswada huo ni kuweka mazingira bora ya usimamizi wa masuala ya usafiri baharini pamoja na kuweka ushirikiano mzuri katika kusimamia sheria kati ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Jamhurri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha marekebisho ya sheria yametoa nafasi ya kuitambua sheria ya mwaka 2001 ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usafirishaji nchi kavu na baharini (SUMTRA) ambao watafanyakazi kwa kushirikiana na mamlaka ya usafirishaji Zanzibar (ZMA).

Marekebisho hayo yamekuja baada ya ajali mbili za meli kuzama katika mwambao wa Zanzibar na kupoteza mamia ya wananchi.
 
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment