Geremia Kulwa (45) mkazi wa Kata ya Kunduchi Jijini Dar es Salaam akitoa maoni yake mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Amependekeza watendaji katika ofisi za umma wasizigeuze ofisi hizo kama kampuni zao binafsi bali wawahudumie wananchi kwa haki (Picha na Matern Kayera)
Jumapili,Decemba9 2012.
KWA UFUPI
“Hakujawahi kuwepo kwa nchi inayoitwa Tanzania Bara wala Tanzania Visiwani. Haya ni mapungufu ambayo Katiba Mpya inatakiwa kuyarekebisha ili historia ibaki kama ilivyokuwa. Tanganyika itambulike kwa kuwa Muungano uliopo ni kati ya nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar,” anasema Adventina Ndibalema mkazi wa Kimara Korogwe.

Katika Sura ya Kwanza, Ibara ya (1) na Ibara ya 2(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 zinaeleza maana ya Muungano. Ibara hizo kwa pamoja zinasema kuwa Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. Inaendelea kufafanua kuwa eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
Ibara hizi hazisemi chochote kuhusu nchi za Tanganyika na Zanzibar, bali zimebadilishwa jina na kuitwa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Hapa ndipo wananchi wengi kwenye mikutano ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba wanapotaka Serikali ya Tanganyika irejeshwe kama ilivyokuwa kwa Serikali ya Zanzibar ambayo ipo tangu Muungano uanzishwe, Aprili 26, 1964.
Mwenyekiti wa Chama cha NLD (National League for Democracy) Dk Emmanuel Makaidi ameiambia Tume kuwa Serikali ya Tanganyika iliyouawa wakati wa Muungano inatakiwa kurejeshwa kupitia Katiba ijayo. Dk Makaidi anasema kuwa Wazanzibari katika Katiba yao, wanaitambua nchi yao, lakini Tanganyika haitambuliki mahali popote.Hapa ndipo wananchi wengi kwenye mikutano ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba wanapotaka Serikali ya Tanganyika irejeshwe kama ilivyokuwa kwa Serikali ya Zanzibar ambayo ipo tangu Muungano uanzishwe, Aprili 26, 1964.
Kutokana na sintofahamu iliyopo kuhusu Tanganyika, Dk Makaidi kama ilivyo kwa wananchi wengine anaona kuwa Serikali ya Tanganyika ni haki ya Watanganyika ambayo hainabudi kurejeshwa kupitia mchakato huu wa kurekebisha Katiba ya nchi. Anasema kuwa kuuawa kwa Serikali ya Tanganyika ni kesi ambayo kwa muda mrefu haikupata majibu, lakini sasa majibu yake yapatikane kupitia Katiba ijayo.
“Haiwezekani tuwe kwenye Muungano ambao unaruhusu upande mmoja wa Muungano kuwa na Serikali yake, Bunge lake na kila kitu, halafu upande mwingine uwe umepoteza Serikali na mambo yake yote. Wenzetu wa Zanzibar wanayo Serikali lakini Tanganyika haijulikani iko wapi, ni bora tuungane na Burundi kuliko kuendelea kuwa kwenye Muungano huu,” anasema Abeid Rutozi ambaye kitaaluma ni mkalimani kutoka Kata ya Saranga jijini Dar es Salaam.
“Hakujawahi kuwepo kwa nchi inayoitwa Tanzania Bara wala Tanzania Visiwani. Haya ni mapungufu ambayo Katiba Mpya inatakiwa kuyarekebisha ili historia ibaki kama ilivyokuwa. Tanganyika itambulike kwa kuwa Muungano uliopo ni kati ya nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar,” anasema Adventina Ndibalema mkazi wa Kimara Korogwe.
Katika Sura ya Kwanza, Ibara ya (1) na Ibara ya 2(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 zinaeleza maana ya Muungano. Ibara hizo kwa pamoja zinasema kuwa Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. Inaendelea kufafanua kuwa eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
Ibara hizi hazisemi chochote kuhusu nchi za Tanganyika na Zanzibar, bali zimebadilishwa jina na kuitwa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Hapa ndipo wananchi wengi kwenye mikutano ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba wanapotaka Serikali ya Tanganyika irejeshwe kama ilivyokuwa kwa Serikali ya Zanzibar ambayo ipo tangu Muungano uanzishwe, Aprili 26, 1964.
Hapa ndipo wananchi wengi kwenye mikutano ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba wanapotaka Serikali ya Tanganyika irejeshwe kama ilivyokuwa kwa Serikali ya Zanzibar ambayo ipo tangu Muungano uanzishwe, Aprili 26, 1964.
Mwenyekiti wa Chama cha NLD (National League for Democracy) Dk Emmanuel Makaidi ameiambia Tume kuwa Serikali ya Tanganyika iliyouawa wakati wa Muungano inatakiwa kurejeshwa kupitia Katiba ijayo. Dk Makaidi anasema kuwa Wazanzibari katika Katiba yao, wanaitambua nchi yao, lakini Tanganyika haitambuliki mahali popote.
Kutokana na sintofahamu iliyopo kuhusu Tanganyika, Dk Makaidi kama ilivyo kwa wananchi wengine anaona kuwa Serikali ya Tanganyika ni haki ya Watanganyika ambayo hainabudi kurejeshwa kupitia mchakato huu wa kurekebisha Katiba ya nchi. Anasema kuwa kuuawa kwa Serikali ya Tanganyika ni kesi ambayo kwa muda mrefu haikupata majibu, lakini sasa majibu yake yapatikane kupitia Katiba ijayo.
“Haiwezekani tuwe kwenye Muungano ambao unaruhusu upande mmoja wa Muungano kuwa na Serikali yake, Bunge lake na kila kitu, halafu upande mwingine uwe umepoteza Serikali na mambo yake yote. Wenzetu wa Zanzibar wanayo Serikali lakini Tanganyika haijulikani iko wapi, ni bora tuungane na Burundi kuliko kuendelea kuwa kwenye Muungano huu,” anasema Abeid Rutozi ambaye kitaaluma ni mkalimani kutoka Kata ya Saranga jijini Dar es Salaam.
http://www.mwananchi.co.tz/Katiba/-/1625946/1639912/-/item/1/-/bwdabgz/-/index.html
No comments :
Post a Comment