Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 9, 2012

WARAKA KUTOKA ZANZIBAR: Bila mambo haya CCM hatihati 2015

Na Bila mambo haya CCM hatihati 2015

Posted  Jumatano,Decemba5  2012
KWA UFUPI
IKIWA Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinataka kushinda Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 ni lazima kijirekebisha sasa kwa upande wa Zanzibar.
IKIWA Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinataka kushinda Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 ni lazima kijirekebisha sasa kwa upande wa Zanzibar.
Kijirekebishe kwa sababu mazingira ya uchaguzi yamebadilika, wapiga kura wapya ni wenye matumaini ya maendeleo na kuondolewa matatizo yao ya kijamii, ukosefu wa ajira, maisha bora kwao ndio kipaumbele.
CCM sio tena chama dola, hakilindwi na Katiba kwa kuwa Tanzania ilirejea mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1992, hivyo kudhani kuwa CCM ina hakimiliki ya kutawala milele ni kujidanganya kwa dhamira yake kubaki madarakani, CCM Zanzibar waelewe kuwa dhamira ya kila chama cha siasa kushinda uchaguzi na kuunda Serikali.
Wazanzibari wa leo wengi wao wamezaliwa baada ya mageuzi ya kisiasa, hawamjui Sultan wala Mapinduzi, mambo hayo yamebaki katika kumbukumbu ya matukio ya kihistoria tu.
Ushindi wa chama chochote cha siasa Zanzibar unategemea nguvu ya wapigakura wenye misimamo ya wastani katika siasa kwa ushawishi wa hoja. Chuki, ubaguzi na kutegemea nguvu za dola sio mtaji sahihi kwa chama cha siasa kushinda uchaguzi, kundi lililozuka Zanzibar linalojiona kama lenye haki ya kutawala daima dumu kwa sababu ya jeuri ya dola linajidanganya.
Hawa wanajidai wao ndio CCM kindakindaki, wanaona wengine hawana haki. Wamekuwa wakitumia karata ya kulinda Mapinduzi na utetezi wa Muungano kama ndio ngao yao.
Jambo moja ambalo tunataka kuwaeleza ni kuwa sehemu kubwa ya CCM Zanzibar iliyopo leo, ni tafauti kabisa na ASP. Katu ASP hakikuwa chama cha wababaishaji, mamluki; hakikuwa chama cha wazushi. Waasisi wa ASP akina Mzee Karume, Thabit Kombo Jecha na wengineo walianzisha chama kwa kuamini katika umoja, ndio maana waliunganisha African Association na Shiraz Association.
Waasisi wale wa ASP walitoa mali zao, walitoa thumni zao na wakati wao kwa manufaa ya kizazi cha baadaye cha Zanzibar. Waliwakaribisha watu wa aina na kabila zote ndani ya cham na baada ya Mapinduzi kwenye Serikali.
CCM imerithi utawala kutoka Tanu na ASP. Ni Chama kikongwe, lakini tuwakumbushe CCM Zanzibar kwamba kubaki madarakani kwa kipindi kirefu, kunaweza kukiponza chama kuliko kukisaidia katika mazingira mapya ya demokrasia ya vyama vingi.
Tuwakumbushe CCM Zanzibar kuanguka kwa Chama cha Kanu-Kenya, jifunzeni kutoka kwa Mzee Kenneth Kaunda na Chama chake cha UNIP kilichopigania uhuru wa Zambia.
UNIP kulikuwa na watu na hata Kaunda mwenyewe hakuwa akiamini kuwa ipo siku Wazambia watakikataa chama hicho, Mwaka 1992 uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, yeye pamoja na UNIP yake walishindwa na mgeni katika uwanja wa siasa, mwanamageuzi Frederick Chiluba. Hiyo ni kwa sababu Wazambia walikuwa wamekwisha choka na wimbo ule ule ule, walitaka maendeleo na sio ngonjera za kihistoria na kupigania uhuru, uhuru bila shibe hauna maana kwao.
Ni funzo wanalotakiwa kupata hawa wanaojidai CCM ndio yenye hakimiliki ya kutawala Zanzibar. Ukizitazama nyuso za wapigakura wengi utabaini kuwa Wazanzibari wamechoka kiuchumi wanataka mabadiliko ya maisha yao, kwa hiyo mgombea urais atakayejitokeza mwaka 2015 akawajaza matumaini yenye kuingia akilini wapigakura, bila shaka kilichotokea kwa vyama vya Kanu, UNIP na vyingine ndicho kitakachoikumba CCM.
Kisipojirekebisha kitakabiliwa na hali ngumu, kwani hali ya mambo kwa miaka hii ya karibuni kuongezeka kwa wapigakura wapya kuna kila sababu ya kuamini kuwa siku za kutamba kwa CCM Zanzibar na mahafidhina zinakaribia ukingoni. Wazanzibari wamechoka na hadithi za Hizbu, ASP, Sultan  au Waarabu, Waafrika; watu sasa  wanataka mabadiliko ya maisha yao kutoka hali duni kuwa angalau na uhakika wa mlo wao.
Matokeo ya Uchaguzi uliopita yanapaswa kutazamwa kwa makini sana na CCM kwani imetokea kwenye tundu ya sindano. Kimepoteza majimbo matatu Unguja – Nungwi, Mtoni na Magogoni. Hili ni pigo kwa chama hicho ambacho ngome yake kuu imeanza kumeguka kupitia uchaguzi mkuu mwaka 2010. CCM Zanzibar walipaswa kujitazama upya badala ya kushabikia makundi, chuki na siasa zile zile za tishio la kurejea Sultan ambalo halifanyi kazi tena, limesha-expire kwa sasa.
Lakini badala ya kutafuta njia ya kujihakikishia kubaki madarakani CCM Zanzibar, makundi ndio mwelekeo mbadala wake. Kuna kundi la CCM mahafidhina, CCM maslahi na CCM progressive.
Inaonekana CCM Zanzibar inapita katika kipindi kigumu na kama itavuka salama katika hali ya makundi iliyonayo,  basi kitakuwa na maisha marefu kutawala Zanzibar, kinyume chake ndio mwanzo na mwisho wa mahafidhina na tambo zao.
Siasa za kileo zinahitaji ujuzi, maarifa, sera zenye kuwavuta wapigakura; matamshi ya ubaguzi, ubabe, vitisho havisaidii kukipa ushindi chama cha siasa.
Mtihani mwingine wa CCM Zanzibar ni suala zima la mabadiliko katika muundo wa Muungano. Wazanzibari wengi wanaonekana kutaka yafanyike mabadiliko ya msingi katika muundo huo.
Muundo wa Muungano hauwezi kuendelea kubaki kama ulivyo. Lazima wanasiasa wakubali kwamba matatizo ambayo yanatokana na mfumo wa Muungano  huu hayataweza kuondolewa kwa vikao vya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais, wataendelea kukaa kila siku, lakini hakuna liwalo.
Msimamo wa kutaka mabadiliko ya muundo wenye maslahi kwa maana ya mkataba wenye kuzingatia mfumo wa Serikali mbili zenye dola zinazojitegemea, utakuwa ndio dawa na suluhu ya zile zinazoitwa kero za Muungano.
Wazanzibari maskini wanazungumzia hali ngumu ya uchumi inayoikabili Zanzibar na kuwa ugumu wa maisha unasababishwa na mfumo mbaya wa Muungano. Mathalan,nionavyo mimi Zanzibar ilipojiunga na OIC sio kwa kutafuta kuongeza idadi ya waumini wa Kiislamu kwani tayari asilimia 95 ya watu wote ni Waislamu, ilikuwa njia kuinusuru na dhiki waliyonayo wananchi wake.

Kama sera za kiuchumi za Serikali ya Muungano zinakuwa zinainufaisha Zanzibar kuwa na viwanda  ambavyo bidhaa zake zinauzwa nje, vyenye uwezo wa kuajiri watu 200,000 na kila mtu alipwe mshahara wa Sh300,000 kila mwezi, kutakuwa na  zaidi ya Sh10 bilioni katika mikono ya Wazanzibari.
Ufikapo mwisho wa mwezi kila mtu anakimbilia dukani, marikiti na sehemu nyingine kutafuta mahitaji, mwenye kununua samani, nguo nzuri, mchele wa basmati, pishori au siagi ya kismayuu ataweza, lakini pia hata viwanda vidogo navyo vitachipuka na kufanya mzunguko wa pesa kuwa mkubwa.
Wazanzibari wengi sasa ni maskini hawana uwezo wa kusomesha watoto wao katika vyuo vikuu vyenye hadhi kubwa duniani, ikiwa Boflo, kimbilio la wanyonge haishikiki, imepanda bei nani ataweza kumpeleka Oxford University, University of Edinburgh?

Wazanzibari kwa muda mrefu wamepumbazwa na kauli za mtaji wa maskini ni nguvu zake, katika zama hizi za sayansi na teknolojia masuala ya nguvu kuwa mtaji hayana nafasi tena, akili na ujuzi ndio wenye kuhitajika.
Lakini utapataje ujuzi ikiwa mtoto wako anashindwa kupata elimu bora? Wakati tulionao elimu ndio mtaji wa maskini, lakini tujiulize kuna vyuo vikuu vingapi hapa Zanzibar, mbona Serikali ya Muungano haijengi vyuo vikuu zaidi ya kuweka tawi la utafiti wa sayansi za bahari ambapo watumishi wanaletwa kutoka Tanganyika, Wazanzibari wataambulia ‘uwochimeni’, maana dereva pia katoka kwa kaka mkubwa, vyuo vinajengwa Dodoma, Mwanza, Tanga, Moshi, Arusha na mika mingine.
Asilimia kubwa ya Wazanzibari wanaishi kwa kutegemea jembe la mkono, kipato wanachopata kutoka katika kilimo cha aina hiyo sote tunakijua hakiwasaidii kukidhi mahitaji yao muhimu ya kila siku seuze kuendelea, kwa sasa walio wengi wanaishi chini ya mstari wa umaskini.
Hakuna jambo la kufichana, mfumo wa Muungano wa kikatiba umeshindwa na ndio umetufikisha hapa tulipo.
Wengi wanadhani muundo wa Muungano  ungekuwa kama ule wa Muungano  wa Ulaya kila mtu na chake, tunashirikiana kwa baadhi ya mambo ingekuwa vizuri zaidi kuliko mambo yalivyo sasa. Ni jambo lililo wazi kuwa Muungano wa kikatiba kinga yake ni CCM kuendelea kutawala.

http://www.mwananchi.co.tz/kolamu/Waraka-kutoka-Zanzibar/-/1614862/1636944/-/item/1/-/t6tjr9z/-/index.html

No comments :

Post a Comment