Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini, Borafya Silima, leo katoa maoni yake katika Uwanja wa Alabama, Shehia ya Miembeni. Katika maoni yake kasema anataka Serikali Mbili, ya Muungano na ya Zanzibar, lakini kila Serikali iwe na mamlaka yake kamili. Akasema pia anataka waendelee kuwepo Marais wawili, wa Muungano na wa Zanzibar, lakini wote wawili wawe na hadhi sawa na wawe na mamlaka kamili. Akamalizia kwa kusema anahimiza umoja na mshikamano.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment