Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 6, 2012

Mtaalam aeleza kwanini Tanzania ni maskini


NA ASHTON BALAIGWA

6th December 2012

Imeelezwa kuwa kasi ndogo ya kupungua kwa umasikini nchini inatokana na sekta zinazoendesha uchumi kutoajiri watu wengi.

Hayo yamesemwa na Mshauri Mwelekezi wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Deo Mtalemwa, wakati akizungumza katika warsha ya siku moja ya kutoa maoni ya wadau wa serikali za mitaa na asasi za kiraia juu ya malengo ya milenia (MDG), mjini hapa jana.

Mtalemwa ambaye amefanyakazi na Benki ya Afrika (ADB) kama Afisa Mikopo na Afisa Uhusiano kwa miaka 20, alisema sekta za msingi zinazoendesha uchumi wa nchi kama vile, madini, viwanda, ujenzi na utalii zimeajiri idadi ndogo ya Watanzania ikilinganishwa na sekta ya kilimo ambayo licha ya kuajiri idadi kubwa ya watu lakini imekosa msukumo wa kutosha kuchangia ukuaji wa uchumi.

Sababu nyingine alizotaja kukwamisha jitihada za Tanzania kupunguza umasikini ni, kuwepo kwa migawanyo mibovu ya rasilimali za nchi, baadhi ya mikoa kuwa na rasilimali nyingi na mingine ikiwa haina rasilimali za kutosha na kuwepo kwa mifumo mibovu ya ukusanyaji kodi na usimamizi wake.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo, ni lazima Tanzania ikapanua wigo wa ukusanyaji kodi ili Watanzania wote walipe kodi na kutolea mfano wa posho za vikao mbalimbali kuwa zimekuwa zikitolewa pasipo kukatwa kodi jambo ambalo alidai ni eneo jingine linaloweza kupanua wigo wa kodi.

Aidha, Mutalemwa aliwataka Watanzania kutotumia njia za ujanja ujanja kukwepa kodi badala yake walipe kodi kwa hiari ili kujenga ujasiri wa serikali wa kuhoji pale ambapo wanaona matumizi ya fedha zao hayafanywi kwa usahihi.

Hata hivyo, alisema Tanzania imefanya vizuri katika kukuza uchumi wake kutoka asilimia 6.8 mwaka jana hadi kufikia asilimia 7.1  mwaka huu.

Alisema utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa umebaini kuwa, umasikini nchini umepungua kwa asilimia 5 katika kipindi cha miaka 18 toka mpango wa milenia wa kupunguza umasikini duniani ulipopitishwa na mataifa 189 Tanzania ikiwemo na kuanza kufanyiwa kazi mwaka 1994 mpaka sasa.

Takwimu za umoja huo zinaonyesha uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia 7.1 mwaka huu toka asilimia 6.8 mwaka 2011, huku Uganda ikionyesha uchumi wake kukua kwa kasi zaidi kwa toka asilimia 4.1 mpaka kufikia asilimia 6.0.

Nchi nyingine katika ukanda wa Afrika Mashariki ni Rwanda ambayo uchumi wake umekua kwa asilimia 9.9 kutoka asilimia mwaka 2011 hadi asilimia 8.8 mwaka huu, huku Burundi ukikua kwa 4.8 mwaka huu toka  asilimia 4.2 mwaka jana.

Kwa upande wa Kenya, uchumi wake unaonyesha kushuka kwa asilimia 1.6 kutoka asilimia 5.1 mwaka jana hadi asilimia 3.5 mwaka huu.


CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment