Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 19, 2012

Pinda atangaza amri 10 za kuendeleza kilimo

18 Dec 2012.

Na Mwandishi Wetu, Katavi 

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, juzi amefanya ziara ya ghafla na kukagua mashamba ya viongozi mkoani Katavi kwa kuanza na shamba la Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Rajab Rutengwe.


Shamba jingine alilokagua Bw. Pinda ni la Katibu Tawala wa Mkoa, Mhandisi Emmanuel Kalobelo, ambapo mashamba yote yako katika Kijiji cha Songambele eneo la tankifupi, Kata ya Nsimbo, Wilaya ya Mlele, mkoani humo.

Dkt. Rutengwe ana shamba la ekari tano ambalo limepandwa mahindi na linatumika kama shamba darasa wakati Mhandisi Kalobelo ana shamba la ekari nne na nusu alilopanda mahindi
pamoja na miembe ya kisasa.

Mbali ya kukagua mashamba hayo, Bw. Pinda alizungumza na wakazi wa Kijiji cha Songambele na kuwatangazia amri 10 za kuendeleza kilimo, katika Wilaya na Mkoa huo.

Bw. Pinda ambaye alikuwa katika siku ya tano ya ziara yake jimboni kwake Katavi, wilayani Mlele, alisema amelazimika kuandaa amri hizo kwa kutambua kwamba, kila mtu anahitaji kula chakula bila kujali ni kiongozi wa ngazi ya juu au mwananchi wa kawaida.

“Tumbo halijali wewe ni Waziri Mkuu, mwalimu, Mkuu wa Mkoa au askofu, njaa ikiuma linataka kulishwa, kama kila mtu anahitaji kula, lazima tulime na katika hili, watoto, wagonjwa na wazee
ndio ambao tutawasamehe,” alisema Bw. Pinda na kuongeza kuwa,
wapo baadhi ya walemavu wanaoweza kulima hivyo nao walime.

Alisema ameandaa amri 10 za kuharakisha maendeleo ya Mkoa huo ambazo ni kila mtu lazima ale, aondokane na umaskini, mwenye uwezo wa kufanya kazi ni lazima alime, awe na ekari moja ifikapo mwaka 2013 na maandalizi ya shamba yaanze mapema.

“Ekari hizi ziwe zinaongezeka kila mwaka ekari moja, yaani mwaka 2014 mtu awe na ekari mbili na mwaka 2015 awe na tatu, mkifanya hivyo mtaona matunda yake,” aliongeza.

Alitaja amri nyingine kuwa, kila ekari itakayolimwa lazima iwe imepimwa kitaalamu, iwe na ukubwa wa hatua 70 kwa 70, ilimwe kwa sesa sio matuta, ipandwe kwa kutumia mbegu bora, mistari na kwa kuzingatia nafasi wanazoelekeza wataalamu.

“Ni lazima ekari moja ikupe miche 16,000 ya mahindi, nalisemea hili kwa uchungu kwani nimetembea maeneo mengi nchini na nje kuona jinsi wenzetu walivyoendelea kutokana na kilimo.

“Panda ekari yako kwa kutumia mbole ya minjingu mazao ambayo haiitaji kuongeza mbolea ya kukuzia na mazao yapandwe kwenye mstari kwa kutumia kamba,” alisema Bw. Pinda.

Aliongeza kuwa, amri ya nane lazima palizi ifanyike kwa wakati
na kusisitiza baada ya kuvuna mazao yahifadhiwe ghalani ambapo amri ya 10, alizitaka Halmashauri za Mkoa huo, kuhakikisha kila kijiji kinatunga sheria ndogondogo za kuwasaidia wananchi kutekeleza amri hizo.

Aliwataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani humo waanze kuwa mfano kwa kuwa wakulima wa kwanza ili waweze kuisimamia Serikali itekeleze yale aliyoazimia.

Jana Bw. Pinda alikwenda katika Kata ya Majimoto ambako atapokea taarifa ya mnada, kuzungumza na wananchi.


Chanzo: Majira

No comments :

Post a Comment