Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 19, 2012

Serikali: Tunachukua hatua za kumiliki makaa ya mawe

18 Dec 2012.


Na Stella Aron

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema Serikali inajipanga kuchukua hatua za kumiliki
hifadhi yote ya madini ya makaa ya mawe yaliyopo nchini.


Taarifa iliyotolewea na Wizara hiyo, imesema Prof. Muhongo aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na watendaji kutoka Kampuni ya Sichuan Hongda ya China.

Watendaji wao walimtembelea ofisini kwake wakiongozwa na Balozi wa China nchini, Bw. Lu Youqing ili kujadili masuala mbalimbali yanayoigusa sekta ya nishati nchini ukiwemo
mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma.

Katika mazungumzo hayo, Balozi Youqing aliweka wazi kuwa, katika mradi huo kampuni ya Sichuan Hongda inatarajia kuzalisha umeme wa megawati 600 ambapo kati ya hizo, megawati 400 zitaingizwa katika gridi ya Taifa ifikapo 2018 na megawati 200
zitatumia kuendeshea mitambo.

Kwa upande wake, Prof. Muhongo alisema madini yote ya kimkakati yakiwemo makaa ya mawe, yanapaswa kuwa chini
ya umiliki wa Serikali ili iweze kudhibiti uvunwaji na biashara
yake kwa manufaa ya Watanzania.

“Taratibu zote zikikamilika na Serikali kutwaa umiliki wa hifadhi ya madini haya, itaweza kudhibiti matatizo mbalimbali yanayojitokeza katika sekta hii likiwemo la baadhi ya wamiliki wa maeneo yenye madini hayo kuyashikilia kwa muda mrefu wakisubiri kuingia ubia na wawekezaji wengine au kuyauza nje ya nchi,” alisema.

Alisema hali hiyo inachangia watu makini wenye nia ya kuwekeza katika maeneo hayo kushindwa kufanya hivyo kwa kukosa maeneo  hivyo kuchelewesha maendeleo kwa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Prof. Muhongo aliliagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kufanya mazungumzo na kampuni hiyo ili mradi huo uanze mara moja.

Aliongeza kuwa, mradi huo umechukua muda mrefu bila kuwa na mafanikio hivyo umefika wakati wa Watanzania waone mradi huo ukianza kutekelezwa ili wafaidi matunda yake.

“Pia nimeiagiza TANESCO ifanye mazungumzo na kampuni hii kuhusu ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme kutoka Mchuchuma hadi Mbeya.

“Suala la uzalishaji umeme lazima liendane na uboreshaji miundombinu ya usafirishaji na usambazaji ili kupata
matokeo chanya,” alisema Prof. Muhongo.


Chanzo: Majira

No comments :

Post a Comment