Na Eliasa Ally, Iringa
Kauli hiyo ya serikali ilitolewa jana na Waziri wa Fedha Dr William Mgimwa wakati akizungumza na Majira mjini Iringa mara
baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi 29 katika ukumbi wa Maendeleo wa Hall Fair uliopo eneo la Kitanzini mjini Iringa ambapo vikundi hivyo vilivyoko mkoani hapa vinavyofadhiliwa na mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Iringa Bi, Ritta Kabati wa
chama cha mapinduzi (CCM).
"Serikali imeanza kufuatilia wale wote walioweka fedha nje ya nchi na endapo watabainika kuwa fedha hizo wameziweka kwa njia haramu, serikali inafutilia kwa karibu kwa kuwasiliana na nchi husika ambazo zinatajwa kuwa fedha hizo zimewekwa na kudaiwa kuwa ni za mafisadi ndiyo wanaweka fedha hizo na serikali haina hofu na kundi au mtu wanaosemekana wanaweka fedha katika mabenki ya nje ya nchi",
alifafanua Dkt. William Mgimwa.
Aliongeza kuwa watu hao ambao wanaoficha fedha nje ya nchi wanasababisha uchumi wa ndani ya nchi kuzidi kudidimia ambapo alisema kuwa dawa ya watu hao ipo jikoni inachemka ambapo alisema kuwa serikali inashindwa kuwaelewa watu hao sababu za kuficha fedha hizo nje ya nchi na kuhoji kuwa kwa nini wasiweke fedha hizo ndani ya benki za hapa nchini ili kukuza na kuongeza mapato ya serikali kitu ambacho kitaleta faida kubwa.
Dkt William Mgimwa alisema kuwa hatua hiyo ya serikali ya kutangaza uamuzi huo imekuja kufuatia vitendo vya baadhi ya watu kujilimbikizia fedha nyingi huku wakihamisha kutoka ndani ya nchi na kupeleka kwenye mabenki ya nje ya nchi na kuwa serikali itawabana wale wote wanaoficha fedha nje ya nchi na kutaka fedha hizo
kurejeshwa nchini.
Aidha, aliwataka wale wote ambao wanahusika na kuficha mabilioni ya fedha nje ya nchi kuwawazi na watoe maelezo malengo yao ya kuziweka fedha hizo nje ya nchi ili kuondoa malamiko mbalimbali ambayo yanatokea kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuhusiana na swala hilo.
Chanzo: Majira
No comments :
Post a Comment