Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 20, 2012

TANESCO yatangaza neema kwa wateja

19 Dec 2012

Na Stella Aron

SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO), limepunguza gharama
za kuunganisha umeme kwa wateja wapya kuanzia Januari 2013
ili wananchi wengi waweze kupata huduma hiyo ifikapo 2015.


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam juzi na Meneja Mawasiliano wa shirika hilo, Bi. Badra Masoud, ilisema Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Bunge la Bajeti, mjini Dodoma,
mwaka huu, alitaja gharama mpya za kuunganisha umeme.

Alisema lengo la shirika ni kupunguza gharama za kuunganisha umeme wa njia moja kwa asilimia 30 (wateja wadogo mijini), na
punguzo la wastani wa asilimia 70 kwa wateja wa vijijini.
Aliongeza kuwa, gharama kwa wateja ambao watajengewa njia moja kwenye umbali usiozidi mita 30 bila kuhitaji nguzo katika maeneo ya vijijini watalipa sh. 177,000 na mijini sh. 320,960 badala ya sh. 455, 108 zinazolipwa sasa.

Bi. Masoud alisema punguzo hilo ni sawa na asilimia 61.11, kwa wateja wa vijijini na asilimia 29.48 kwa wateja wa mijini.

“Wateja ambao watajengewa njia moja na kuwekewa nguzo moja katika maeneo ya vijijini watalipa sh. 337,740, mijini sh. 515.618 badala ya sh. milioni 1, 351,884 zinazolipwa sasa na wateja,” alisema.


Aliongeza kuwa, wateja ambao watajengewa njia moja na kuwekewa nguzo mbili katika maeneo ya vijijini watalipa sh. 454, 654 na mijini sh. 696, 670 badala ya sh. 2, 001, 422 ambazo zinalipwa na wateja kwa sasa.

Alisema vifaa mbalimbali vya kuunganisha umeme kwa wateja wapya vimewasili katika mikoa na Wilaya mbalimbali nchini.

Chanzo: Majira

No comments :

Post a Comment