Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 4, 2012

Wanawake CCM sasa wasakamana


NA CYNTHIA MWILOLEZI
4th December 2012

Makundi bado yanakitafuna Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha, baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama hicho mkoa huo, Flora Zelote, kudaiwa kumshambulia Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige, kuwa misaada aliyoitoa wiki iliyopita ina lengo la kutaka ubunge kupitia jumuiya hiyo mwaka 2015.

Hatua ya Zelote ya kumshambulia Magige inafuatia kitendo cha mbunge huyo wiki iliyopita cha kutoa msaada wa baiskeli 20 kwa walemavu zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. milioni nane.

Mbunge huyo kupitia Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM), alitoa msaada huo baada ya kuzindua taasisi yake ya kusaidia vijana, wanawake na watoto ijulikanyo kwa jina la “Chatherine Foundation Development” yenye makao yake makuu jijini Arusha.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao cha Baraza la UWT Mkoa wa Arusha kilichofanyika Arumeru Novemba 30, mwaka huu, zinasema kuwa Zelote ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Musa Wilaya ya Arusha, alimshambulia Magige na kuwaeleza wajumbe kuwa mbunge huyo hana jipya kwani misaada anayotoa ni ya kutaka kujijenga ili aweze kupata ubunge mwaka 2015 kupitia UWT.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Zelote alisema katika kikao hicho kuwa anamtambua mbunge mmoja tu wa Viti Maalum mkoani Arusha ambaye ni Namelok Sokoine, mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine.

Aidha, habari zinasema kuwa Zelote alihamasisha wanawake kutohudhuria uzinduzi wa taasisi ya Magige.

Vyanzo vya habari vinasema kuwa Zelote aliwaeleza wajumbe kuwa hawana sababu ya kuhudhuria kwa kuwa kazi inayofanywa na mbunge huyo (Magige) siyo ya wanawake, bali ni ya walemavu na yeye (Zelote) asingehudhuria kwa sababu hizo.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu ili kutoa ufafanuzi wa kuhusiana na suala hilo, Zelote alithibitisha kutohudhuria katika shughuli hiyo kwa maelezo kuwa ilikuwa ya wenye ulemavu na siyo ya UWT.

Pia, Zelote alithibitisha kusema kuwa anamtambua Namelok Sokoine kuwa ndiye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha.

Hata hivyo, alipoulizwa kwa nini hamtambui Magige kuwa Mbunge wa Viti Maalum, alijibu kuwa hamtambui kwa kuwa anatokana na UVCCM na siyo UWT anayoiongoza.

Kuhusu madai kuwa alisema misaada ya Catherine ni ya kujijenga kutaka ubunge mwaka 2015 kupitia UWT, Zelote alikana kutoa kauli hiyo na kufafanua kuwa alichokisema ni kuwa ilikuwa misaada kwa ajili ya wenye ulemavu na jamii nyingine.

“Kweli ninayemtambua ni mbunge mmoja tu Namelok Sokoine wa Viti Maalum mkoa wetu (Arusha) na siyo mbunge mwingine na nitaendelea kuamini hivyo siku zote, ila kuhusu misaada ya Magige kuwa ni kampeni ya ubunge kupitia UWT siamini hivyo,” alisema.

Magige alipoulizwa kuhusu tuhuma za kushambuliwa na Zelote, alithibitisha kuzisikia na kueleza kuwa kutoa kwake misaada ni kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM kwa jamii inayowazunguka na siyo kampeni za ubunge.

Alisema kwa sasa Rais, Dk. Jakaya Kikwete na ndiye anayemheshimu na kumsaidia katika kutekeleza ilani ya CCM mpaka mwaka 2015 atakapopatikana Rais mwingine.

“Rais ajaye wa mwaka 2015 hakuna mtu anayemjua kwani ni Mungu pekee ndiye anayemjua na kama wao wanaye Rais wao, waendelee kuamini hivyo, lakini hilo kwangu halipo,’’ alisema Magige.

Akizungumzia kutaka kuwania ubunge kupitia UWT Mkoa wa Arusha, Magige aliwataka wanawake kusubiri muda ufike ili kila mwenye sifa ya kugombea agombee kwa kuwa ni haki ya kila mwana chama wa CCM.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment