Written by ibnially // 04/12/2012
Wazanzibar na waislamu kwa ujumla wametakiwa kushajihishana mambo ya kheri ili kuweza kuupeleka mbele uislamu.
Hayo yameelezwa na kiongozi wa harakati za daawa nchini uingereza{IERA} duktuur Yussuf Chamber alipokua akizungumza na wanafunzi pamoja na waislamu walohudhuria katika mhadhara uliofanyika katika chuo kikuu cha elimu chukwani.
Amebainisha ya kwamba wajibu wa binaadamu kuletwa duniani ni kumuabudu M/Mungu lakini wanaadamu wanajishau na kujiingiza katika masuala yasiyo ya maana ikiwemo kushabikia mpira na kuufanya ndio mungu wao.
Ameongeza kwa kusema kuwa hizo mbinu maaalum za wasioupenda uislamu katika kuubomoa uislamu na kueneza dini zao hivyo amewataka waislamu kuwa makini na dini yao na kufundishana mambo mema ili kuweza kuisimamisha dini ya kiislamu.
Aidha Dr Yussuf ameahidi ya kwamba ifikapo mwezi wa February 2013 atakuja tena Zanzibar kwa ajili ya kuanzisha chuo maalum ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo ya kuhubiri uislamu.
Na kwa baadhi ya waliohudhuria katika mhadhara huo wameelezea kufurahishwa na ujio wa dr Yussuf kwani umeweza kuleta manufaa na sura mpya kwa waumini wa kiislamu.
Mhadhara huo wa Dr Yussuf ni muendelezo wa mihadhara yake ambayo anaifanya katika nchi tofauti za afrika na ulaya.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment