Mosque
Church
19 Dec 2012.
kwenye warsha iliyolenga kujadili dhamana waliyonayo katika kudumisha, kulinda amani na utulivu uliopo nchini.
Mgeni rasmi katika warsha hiyo alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Katika mkutano huo, viongozi hao waliitaka Serikali kuona umuhimu wa kushirikisha wananchi katika utungwaji wa Katiba
Mpya na kuhakikisha mambo yote yanayoendeleza umoja na
mshikamano yanaingizwa katika katika hiyo.
Maazimio yaliyofikiwa na viongozi hao ni pamoja na kuitaka Serikali itekeleze majukumu yake kwa kuhakikisha haki
inatendeka, sheria, kanuni na taratibu zinafuatwa pamoja
na kulinda rasilimali zilizopo kwa manufaa ya Taifa.
Viongozi hao walidai kuwa, wajibu walionao kwa jamii ni kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uadilifu na kujiheshimu
ili kuleta utulivu na mshikamano wakati wote.
Hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete aliwaonya watu wanaotumia kivuli cha dini kutaka kuvuruga amani iliyopo nchini na kusisitiza Serikali ipo makini kuhakikisha mtu yeyote ambaye atajaribu kuwaweka Watanzania roho juu, atachukuliwa hatua bila kujali
ni nani na anatoka wapi.
Alisema ni aibu kufanya vurugu hasa ukizingatia kuwa, Watanzania wamelelewa katika misingi ya upendo, kuheshimiana, mshikamano na uadilifu ambapo kazi hiyo ilifanywa na waasisi Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume.
Sisi tunasema kuwa, vurugu zinazotokana na kivuli cha dini, zinachangia kuidhalilisha nchi na Watanzania kwa ujumla.
amani ya Tanzania ndio sifa kubwa tuliyonayo katika mataifa mbalimbali duniani na ndio msingi wa ongezeko la watalii, wawekezaji na ukuaji wa uchumi wetu.
Ukweli ni kwamba, amani ni bidhaa adimu kuliko petroli na
umeme. Hatuwezi kukopa amani hivyo jambo la msingi kwa
kila Mtanzania kuilinda na kuithamini kwa nguvu zote bila
kujali dini yake, kabila wala rangi.
Viongozi wa dini wana dhamana kubwa ya kuhubiri amani ili iendelee kuwepo na kuchochea maendeleo. Taifa lolote ambalo limechezea amani yao lipo katika hali mbaya kiuchumi na raia
wake hawana matumaini ya kuishi maisha bora.
Leo hii Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za kujiletea maendeleo ambazo zinahitaji utatuzi hivyo kama amani tuliyonayo itatoweka, matumaini ya Watanzania kuondokana na kero walizonazo yatakuwa madogo.
Amani ya Tanzania haitadumishwa kwa ngonjera za kusema
nchi yetu ni ya amani bali jambo la msingi ni kuilinda.
Ni vyema Watanzania kutoka makundi yote, Wakristo, Waislamu, Wahindu, dini nyingine, wazee kwa vijana, wake kwa waume wakaelewa kwamba, amani tuliyonayo ni tunu.
Chanzo: Majira
No comments :
Post a Comment