25th December 2012
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika laUmeme Tanzania (Tanesco), Felchesmi Mramba, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa umeme wakati wa sikukukuu za mwisho wa mwaka.
Mramba aliitoa taarifa hiyo baada ya waandishi wa habari kutaka kujua kuhusu maandalizi ya mpango huo ikiwa ni pamoja na vifaa na idadi ya wateja wanaotarajiwa kuunganishwa mara baada ya zoezi hilo kuanza ili kuwaondolea wasiwasi Watanzania baada ya shirika hilo kupeleka maombi yake kwa serikali ya kuongeza gharama za nishati hiyo kwa zaidi ya asilimia 81.
“Bei za kuunganisha umeme zitashuka kuanzia Januari mosi mwakani na kuendelea na sio kwa mwezi huo tu bali hata wale watakaokuunganisha umeme Mwezi Mei na kuendelea wataungansihiwa kwa gharama hizo za punguzo zilizowekwa na serikali,” alisema Mramba na kuongeza:
“Mara baada ya zoezi hilo kuanza tunatarajia kuunganisha takribani wateja 250,000 kwa mwaka 2013. Mwaka jana wateja 24, 000 waliunganishwa na kwa mwaka huu takribani wateja 90,000 wameshaunganishiwa umeme.”
Kuhusu tatizo la kukatikakatika kwa umeme wakati wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya, alisema kuwa shirika hilo limejipanga vyema kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa maeneo yote nchini na kwamba hakutakuwapo na matengenezo yoyote isipokuwa ya dharura tu hadi ifikapo Januari 2, mwakani.
Alisema matatizo ya kukatikakatika kwa umeme yanayoendelea hivi sasa nchini kote, si mgawo bali ni kutokana na matatizo ya kiufundi kwa madai ya kwamba kiasi cha umeme kilichpo kinatoseheleza mahitaji kwa kuwa nishati inayotumika kwa sasa si ya maji pekee bali ni pamoja na ile ya mafuta na gesi.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment