Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 7, 2012

ZANZIBAR AIRPORT: Ombi kwa Wafanyakazi wa Uhamiaji Zanzibar Airport


Written by   //  07/12/2012  

Wafanyakazi wa Uhamiaji {Migration} Zanzibar Airport wacheni Jeuri, Kibri na Choyo, watu wanasafiria kutumia Airport ya Zanzibar watoe visa Mupate Rizki.Pia mtu akiwa na Passport ya Tanzania mwanawe akiwa na ya Nchi nyengine yeyote hamuruhusiwi kumlipisha Visa, anakwenda Migration kumuwekea mwanawe muhuri wa Dual Citizen {bila ya malipo} inayoweza tumika mpaka afike 18..kama sheria inavyosema ” The Tanzania citizenship is governed by the Citizenship Act, 1995. This Act proscribes the right to dual citizenship. S. 7(4) provides”Any Citizen of Tanzania shall cease to be a citizen if having attained the age of 18 years, he acquires the citizenshp of some country other than Tanzania by a voluntary act other than marriage”. Musijizuzue na kuwangangania watu walipe visa na kuwatisha. Kama mtu hajui sheria za Uhamiaji kwanini anakuwa Migration Officer. Hasa pale munapomuona mwanamke ndiye msafiri. Musiwasumbue watu, watashukia Tanganyika muikoseshe Nchi ya Zanzibar rizki na nyinyi mukose kazi.
Watu wapokuwa na Passport za nchi nyengine ikiwa ni ya Oman/Uengereza na kazaliwa Zanzibar au hajazaliwa Zanzibar au anahusu Zanzibar, akilalamikia kitu ambacho ni haki au ukweli ukaanza kumjojea wewe si Mzanzibari tu.. hii inaonesha kuwa hujui kazi yako na huna sifa za kuhudumu wasafiri/wateja. Vile vile hamuheshimu watu mizigo yao munapo ifanyia upekuzi. Kuweni waungwana. Kazi yako isikufanye ukawa jabari.
Mgeni anekuja Zanzibar awe amengia halali na kisheria na amefuata utaratibu ndio matakwa ya Nchi, kuwajojea watu hayakufanyi wewe kuwa mbora mbele ya Mola wako kuliko mwengine akiwa Msomali, Mchina, Muarabu, Mburundi. Fanya kazi yako kisheria na kiungwana waache watu wende na safari zao huo ndio ustaarabu wa Mzanzibari, ukarimu na uungwana.
Asanteni kwakuwa waungwana na kurekebisha tabia.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment